Wajumbe wa katiba zanzibar kulipwa posho zaidi ya wa tanzania bara

Wajumbe wa katiba zanzibar kulipwa posho zaidi ya wa tanzania bara

mshumbue-soi

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2013
Posts
1,842
Reaction score
1,148
Heshima kwenu

Hoja ya wajumbe wa katiba kuacha walichopaswa kujadili KANUNI za kuendesha bunge la katiba na hata kuonyesha kilichowapeleka Dodoma ni katiba kama kipaumbele na sio posho kwa kuwa bunge la kawaida posho yake haifikii waliyopewa licha ya kutaka zaidi.

Imebainika ni kutokana pia na wenzao kutoka Tanzania visiwani kulipwa zaidi ya posho ya laki tatu.

Je? Kwanini wanaotoka Tanzania Visiwani iliamuliwa walipwe zaidi?

Waliofanya maamuzi hayo walikuwa na hoja gani ya msingi ya kuwabagua kwa njia ya tofauti za posho au walitaka wajumbe wajadili sana hata 75 % posho badala ya Kanuni ili mwisho iweje.

Kwa kuwa wanajamvi wana
uwezo wa kuanzia walipoishia na kubaini nia ya mjadala uwe posho badala ya Rasimu.

Kulikoni kuwapa wengine zaidi?

Nawasilisha
 
wa zanzibzr uchumi wao mkubwa walisha zoea posho kubwa kubwa, hivyo wana takiwa ku maintain ze standard
 
Zanzibr tutaendelea kuiburuza tanganyika mpaka ikome,zanzbr kwanza.
 
zenj mtatukubali 2 mpka mwenyekit atatoka huku, hrf kila jimbo litawakilishwa na wabunge wawil wa muungano
 
hili siamini kama lina ukweli kwani posho za wabunge wa Bunge la Katiba linaamuliwa na mtu mmoja tu - Rais wa Jamhuri ya Muungano. Tena bila kushauriana na Rais wa Zanzibar... so kama wanalipwa zaidi inawezekana wanalipwa na serikali yao pamoja na ile wanayolipwa na hazina
 
hili siamini kama lina ukweli kwani posho za wabunge wa Bunge la Katiba linaamuliwa na mtu mmoja tu - Rais wa Jamhuri ya Muungano. Tena bila kushauriana na Rais wa Zanzibar... so kama wanalipwa zaidi inawezekana wanalipwa na serikali yao pamoja na ile wanayolipwa na hazina

Afadhali umeanza kupata akili,naona tayari unaanza kuelewa kuwa kumbe zanzbr ni nchi na ina rais wake,taratiiibu mwisho utaelewa.
 
Kama kuna ukweli kwamba wajumbe toka nchi ya Zanzibar wameongezewa au wanapata posho zaidi kuliko wale wa Tanganyika (kulingana na tetesi za Mh. Ndassa). Je hili halitoshi kuwa changamoto ya kuwafanya wajumbe kila mmoja kutaka nchi yake itambulike? Maana kama sote tu wamoja na twajenga nchi moja, tuko Dodoma kwa lengo moja kwa nini wengine walipwe zaidi na wengine kiduchu ili hali sote tu Watanzania na zote zinatoka hazina moja (Double standards)? Ni kweli inawezekana wajumbe kutofautiana nauli lakini kwa posho ya siku ambayo wajumbe wote wanaishi mazingira yanayofanana (Dodoma) sidhani kama ni sahihi kutofautiana. Kama wabunge wa Bunge la Jamhuri hawatofautiani kwa posho, kwa nini iwe katika hili Bunge la Katiba? Wajumbe toka Zanzibar, wana nini cha ziada kustahili nyongeza hiyo? Na kama serikali (nchi ya Zanzibar) imeamua kufanya hivi kwa nini haikutoa ushauri huo kwa Serikali ya Tanganyika pia ili wote wafikiriwe sawa? Maana hapa ni kusababisha sintofahamu isiyokuwa na sababu na mwisho wa siku ni kusigana kwenye maamuzi. Tuombe MUNGU hili Bunge liishe salama, ila tayari nanusa harufu ya kushikana mashati kama sio wajumbe kutoka nje ya ukumbi!
 
Naona mnabwata tu!
Kwani wajumbe wa Zanzibar wanalipwa kiasi gani?
 
ndo maana tunataka na sisi watanganyika tuwe na serikali yetu
kwani tunanyonywa na kukandamizwa sana sie yaani
nimejisikia vibaya nilivyosikia znz wanalipwa posho mara2
kweli siye tuko wapi jamani?
heshima kwenu

hoja ya wajumbe wa katiba kuacha walichopaswa kujadili kanuni za kuendesha bunge la katiba na hata kuonyesha kilichowapeleka dodoma ni katiba kama kipaumbele na sio posho kwa kuwa bunge la kawaida posho yake haifikii waliyopewa licha ya kutaka zaidi.

Imebainika ni kutokana pia na wenzao kutoka tanzania visiwani kulipwa zaidi ya posho ya laki tatu.

Je? Kwanini wanaotoka tanzania visiwani iliamuliwa walipwe zaidi?

Waliofanya maamuzi hayo walikuwa na hoja gani ya msingi ya kuwabagua kwa njia ya tofauti za posho au walitaka wajumbe wajadili sana hata 75 % posho badala ya kanuni ili mwisho iweje.

Kwa kuwa wanajamvi wana
uwezo wa kuanzia walipoishia na kubaini nia ya mjadala uwe posho badala ya rasimu.

Kulikoni kuwapa wengine zaidi?

Nawasilisha
 
Daaah! Kumbe Kuwa na serikali tatu italipa sana asee!!! Si mmeona, kama ni kweli post hiyo, manake kwa bunge la katiba unalipwa at least na serkali mbili! Moja ya muungano, pili ya unakotoka na tatu ya rais anayeteua wabunge hao!!! Daaah, miezi miwili tu unauaga ufukara.....ha ha haaaaaa!!! Hili bunge liwepo kila Mwaka, unajua kwa miaka michache ijayo watu wengi watakuwa na mitaji mizuri!!!
 
Back
Top Bottom