Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Dr. Mollel alifanyiwa dua maalum ya Kichaga, na wimbo maalumu wa kumuombea Kwa Mungu, huku wazee wakisisitiza kwamba amekuwa "mtoto wa Siha," akisimama imara katika kutetea maslahi ya wananchi wa Siha. Walisema kwa dhati kwamba kazi zake zimejieleza, na hivyo hawana budi kumwambia Rais Samia asisumbuke kuja kuomba kura, kwani wamejizatiti kutoa heshima ya kura kwa wote wawili, Dr. Mollel na Rais Samia.
Diwani wa Kata ya Ivany, Elinisa Kileo, alikumbusha umuhimu wa Dr. Mollel katika maendeleo ya kata yao. Alisema, "Nimezunguka Siha yote na nimeona, na dare to say, Dr. Samia ametupa upendeleo wa pekee katika Wilaya yetu." Aliongeza kuwa hakuna kata isiyo na mradi wa kituo cha afya, na barabara zinapitika, ikionyesha kazi nzuri inayoendelea.
Katika hotuba yake kwa wanafunzi wa shule ya Oshara, Dr. Mollel alisisitiza umuhimu wa elimu na kujituma. "Kwanza niwapongeze, mmefanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne. Wako watakaobahatika kwenda kidato cha tano na vyuo vya kati. Na wale ambao hamtachaguliwa, nendeni mkajaze nafasi za kuomba kusoma bure katika nafasi zilizotolewa na Serikali ya Samia kupitia ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana," alieleza.
Muonekano Mpya wa Jengo la Utawala utakavyokuwa hivi karibuni katika Hospitali ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi Kibong'oto iliyopo Wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro.
Aidha, aliongeza, "Wanafunzi wa sayansi wa kidato cha sita, fanyeni vizuri, mkifanya vizuri mtaona furaha ya Dr. Samia. Kwa mtoto wa kike, ametoa Samia Scholarship ambayo unalipiwa kila kitu, wewe ni kusoma tu tena huko Ulaya. Msichezee hii fursa."Dr. Mollel pia alielezea miradi muhimu inayotekelezwa katika Wilaya hiyo, akisema, "Dr. Samia ametupa pesa za ujenzi wa Chuo cha VETA kikubwa sana hapa Siha, na tumeshaanza kazi. Chuo hiki, kikamilika, kitawachukua vijana wanaosoma masomo ya ufundi. Hii yote ni mapenzi mazuri ya mama yetu Dr. Samia kwa wananchi wake. Pia, mama yetu Samia ametupa shule nzuri na ya kisasa ya wasichana kwa ajili ya masomo ya sayansi katika Mkoa wetu, na imejengwa Siha."
Wanafunzi walimwomba Dr. Mollel kumfikishia salamu za shukrani kwa Dr. Samia, wakisema, "Sio Rais tu bali pia mama yetu. Amefanya kazi kubwa katika shule yetu. Leo ametusaidia katika vitabu, ametusaidia katika huduma za afya. Tukiugua, tukifika hospitali ya Kibongoto, tunatibiwa kwa wakati na kurudi shuleni. Pia ametujengea mabweni ya kulala, na hii imepelekea ufaulu wetu kuwa mzuri sana. Tunashukuru."
Wanafunzi waliongeza, "Na wewe Mh Naibu Waziri na Mbunge wetu, tunakushukuru sana. Umekuwa daraja la kutuvusha haya yote. Ni mapenzi mema kwako kwetu sisi. Tunakushukuru, umefanya kazi nzuri. Sisi wanafunzi tunakushukuru kwa niaba ya wote, tunasema Asante."
Walipokuwa wakizungumza, wanafunzi walisisitiza kwa furaha, "Kwa mara ya kwanza tumejiandikisha katika Daftari la mpiga kura, na tunaenda kumchagua Dr. Samia!"
Dr. Mollel alitaja kuwa wanajenga kituo cha afya Lawate, Kata ya Kirua, na Dr. Samia ameshatusaidia fedha. Alisema, "Ninaendelea na ziara katika kuangalia utekelezaji wa miradi."