Kuna wajumbe wa nyumba kumi. Hawa ni CCM tu walio na utaratibu huu ambao umeanza tangu zama za chama kimoja.
Kisha kuna wajumbe wa serikali ya Mtaa. Hawa hupigiwa kura na watu wote.
Mkanganyiko ni pale unapokwenda serikali ya Mtaa unaulizwa mjumbe wako wa nyumba kumi ni nani na kutakiwa upate barua ya utambulisho kutoka kwake.