Kwa mujibu wa kamishna wa tume ndugu pole pole akiwa itv katika kipima joto amesema katika tume jaji warioba aliwaambia wajumbe wa katiba kua anae taka posho kubwa amwandikie barua mh rais aongeze posho au ajiuzuru ujumbe waletwe wengine
Yaani ukimsikiliza, aisee Tanzania tunaowazalendo wengi tu kama huyu Kamishna Polepole. Anatoa elimu barabarah, kimsingi nimeelimika vya kutosha sana kipima joto cha leo ITV lilikuwa darsa tosha, na watoa mada walikuwa watu walioshiba kwa ufafanuz mujaarab. Nimelala usingiz mwepes kwa ufafanuz murua. Swali la je, Bunge Maalum la Katiba linayo mamlaka ya Kubadili Rasimu ya Pili ya Mabadiliko ya Katiba. Kimsingi halina mamlaka KUBADILI kadri ya ufafanuz wa wadau hao KISHERIA,na hata Wananch wa kawaida waliochangia wanaona halina mamlaka hiyo kwa kuwa hayo yalikuwa ni maoni ya Wananchi ya moja kwa moja. Ila lina MAMLAKA ya kuboresha. Hata hivyo ikiondokea Likabadili kwa mfano Muundo wa Muungano uliowasilishwa na Tume, basi uhalali woote wa kuijadili Rasimu unakuwa hauna maana kwa kuwa Rasimu yote imeundwa kwa concept ya hizo serikali zilizopendekezwa ikiwemo ya Tanganyika. Hivyo Mwanaheria kadia wakiondoa kipengele kimoja tu kwa mfano cha Muundo wa Muungano uliopendekezwa ambacho misingi yote ya Rasimu imebase humo, kasema kuwa KISHERIA kazi yote ya Tume ya Mzee Jaji Warioba itakuwa sifuri au kama walipoteza muda tu. Kama ni kweli busara na hekima ya hali ya juu inahitajika aisee. Tuwe na Utaifa waheshimiwa wajumbe wa Bunge la Katiba ili tujenge maridhiano ya Kitaifa ili mchakato uzae Katiba tuitakayo kama Taifa. Ila nikimalizia kwa maoni yangu Tanganyika yetu naiona ileee yaja! Karibu Tanganyika, Idumu Zanzibar. Udumu Muungano. Mungu ibariki Tanzania( JMT- Idumu milele, mfarakano mwiko)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.