Centrehalf
JF-Expert Member
- Jun 9, 2013
- 509
- 145
Salaam wana jamvi,
Nikiwa miongoni mwa watz wanaohitaji katiba mpya na walioshiriki kutoa maoni ya mapendekezo ya rasimu ya katiba,ni meona ni vizuri niwakumbushe machache wajumbe wa bunge la katiba.
1. Naomba wajumbe wa katiba watambue kuwa wana kazi ngumu itakayobeba mustakabali wa maisha ya vizazi vya watanzania kwanzia sasa.
2. Watambue kuwa nafasi walizopata ni za kihistoria na za heshima katika maisha yao na watanzania kwa ujumla.
3. Watambue kuwa wao sio bora sana mpaka wakapata nafasi hizo kuliko watanzania wengine waliokosa nafasi hizo.
4. Watambue kuwa rasimu iliyo mbele yao sio ya mzee Warioba na tume yake bali ni ya watanzania kutoka pande zote za jamhuri.
5. Watambue kuwa posho wanazolipwa ni za watanzania masikini wasiojiweza katika mambo mbalimbali kama vile elimu,afya nk.
6. Watambue kuwa rasimu hiyo ni mali ya wananchi na wala si ya vyama vya siasa,serikali,ngo's,taasisi,dini au kikundi chochote kile kiwe haramu au halali
7. Itakuwa ni kosa kubwa kwa mjumbe yeyote kupuuza, kudharau, kupindisha au kuuza maoni ya watanzania kwa kiasi chochote cha fedha.
8. Zimetumika pesa nyingi sana kuandaa rasimu iliyopo kwa sasa pesa ambayo ingewapunguzia machungu na makali ya maisha watanzania lakini wakakubali kuendelea kuumia kwa matumaini ya kupata katiba itakayo waletea matumaini watanzania wote ktika nyanja zote.
9. Kumbukeni kuwa kazi mliyopewa ni ya heshima zaidi kuliko kipato.
10. Itakuwa ni aibu kwenu pamoja na vizazi vyenu iwapo kupitia kwenu taifa litapata katiba mbovu,na itakuwa ni heshima kubwa na baraka kwenu taifa litapata katiba nzuri iliyobeba matakwa ya watanzania na sio ya makundi fulanifulini na watakia kazi njema iliyo tukuka.
Mungu wabariki.
Nawasilisha.mungu libariki bunge letu mungu ibariki tanzania