Pre GE2025 Wajumbe Wanawake Kamati za Shehia waleta mabadiliko Shehia za Micheweni, Sera usawa ya Kijinsia bado kitendawili

Pre GE2025 Wajumbe Wanawake Kamati za Shehia waleta mabadiliko Shehia za Micheweni, Sera usawa ya Kijinsia bado kitendawili

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Torra Siabba

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
243
Reaction score
287
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua umuhimu wa kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake.

Uwepo wa sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 na Mkakati wa Utekelezaji wake ya mwaka 2005, unathibitisha dhamira ya wazi ya Serikali ya kukuza usawa wa kijinsia.

Lakini bado Sera hiyo haijatekelezwa ipasavyo, hili limeonekana katika wilaya ya Micheweni, ambayo ina masheha 25, wakiwa wanaume 17 na wanawake wanane (8) pekee.

Hata kwa upande wa wajumbe wa kamati za masheha utafiti umebaini kuwa, wapo 274, ingawa wanaume ni 169 na wanawake ni 105 tu.

MASHEHA WENYEWE WANASEMAJE
Sheha wa Shumbavyamboni Time Omar Said anasema Sera anaifahamu vizuri ndomana baada ya kupata uongozi akaweka wajumbe wanawake
Anasema kamati yake inawajumbe 10 watano wanawake na wanaume watano.

Anasema anampango wa kuongeza idadi ya wajumbe wanawake kwani wanaume ni wavivu kwenye kazi.

Sheha wa Wingwi Njuguni Hadia Omar Dadi, anaeleza kamati yake yenye wajumbe 10, wanaume ni sita (6) na wanawake wanne (4).

Anasema bila ya kuwepo kiongozi mwanamke huwezi kuzijua kero zinazo wakwaza wanawake, kwani ni vigumu kuelezea shida zao kwa wanaume.
WhatsApp Image 2024-10-29 at 12.15.18_a095d9b2.jpg

Siku zote mwanamke anaweza kufanya vizuri popote atakapokuwepo, kwani mama ni mwenye roho ya huruma, anasema.

Suleiman Shaame Hamad sheha wa Sizini anasema kamati yake ina wajummbe 10, wanawake na wanaume wakiwa idadi sawa.

Anasema unapompa nafasi yoyote mwanamke ni rahisi, kufanikiwa, kwani wao ni wachapakazi na ni washauri wazuri hasa katika nyanja za maendeleo.

Binafsi nimeona nilipowashirikisha wanawake katika kamati yangu, maendeleo yamepatikana, ukulinganisha na hapo nyuma,anafafanua.

Hata kamati ya shehia ya Bopwe Wete, nayo ni mfano mzuri wa utekelezaji wa sera, kwa kuwepo idadi ya wajumbe sawa ya watano kati ya wanawake na wanaume.

shehia ya Ngambwa bado Sera imewapa kichogo maana Shehia inawajumbe 12 lakini kuna wanawake wanne.

WANAKAMATI
Mwanamke siku zote ndio mchapa kazi zaidi kuliko mwanamme, Ali Omar Ali mwanakamati ya Sheha wa Wingwi Njuguni anasema Sera ya Maendeleo ya Jinsia imetekelezwa ipasavyo katika Shehia yao, kwani hata Sheha wao ni mwanamke.

Licha ya kuwa sheha wetu ni mwanamke lakini mabadiliko tunayaona, hana ubaguzi wa chama, Rangi wala Jinsia anafahamisha.

Time Juma Said mkaazi wa Bopwe anasema licha ya kamati yao kuwa na wajumbe wengi wanawake lakini haijawahi kupoteza kitu.

Anasema zamani kamati ilipokua na wajumbe wengi wanaume ilikua na matatizo mengi ikiwemo utoro wa wanafunzi Maskulini.

KATIBA YA ZANZIBAR
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kifungu cha 10 (e) kimeleza kila raia atakuwa na haki sawa, majukumu na fursa sawa kwa mujibu wa sheria.

Ijapokua katiba imeweka usawa kijinsia katika nyanja mbali mbali ikwemo katika vyombo vya maamuzi, na pia nafasi za utendaji, lakini usawa huo haujazingatiwa ipasavyo.

Kwani Zanzibar inayo majimbo 50 ya uchaguzi, ingawa kwa mujibu wa ripoti ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, wawakilishi wanaume ni 42 na wanawake ni wanane (8) tu.
WhatsApp Image 2024-10-29 at 12.16.23_b7785550.jpg

WANAHARAKATI
Afisa Mkuu wa mahusiano kutoka Chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Zanzibar -TAMWA Safia Ngalaphi, anasema licha ya kuwa hawana utafiti rasmi lakini bado Sera ya Maendeleo ya Jamii na Jinsia, haijatekelezeka ipasavyo.

Tukiangalia kwenye ngazi za shehia idadi ya masheha wanawake ni kidogo kwani ni 81 sawa na asilimi 20 kwenye shehia 388 ya masheha wote Zanzibar, anaeleza.

Anaeleza kuwa wanatamani Sera yengetekelezwa, kwani siku zote wanawake ni wapenda amani, wapenda maendeleo na waadilifu kwenye uongozi.

Hafidh Abdi Saidi kutoka jumuiya ya Utetezi wa Kimazingira na Jinsia PEGAO ambapo yeye anasema kwa baadhi ya tasisi tayari wamekuwa na uwelewa wa kuitekeleza Sera.

Tukiangalia hata kwenye kamati ya Tume ya Uchaguzi ya Bara ambayo imeundwa imezingatia usawa wa kijinsia, kwani ina wajumbe 19, wanawake 12 na wanaume Saba tu.

JAMII
Bimize Othman mkaazi wa Shumba mjini anasema katika Shehia yao Sera imetelezeka maana hata Sheha wao ni mwanamke.

Tunajivunia kupata kiongozi huyu mwanamke kwani tunauwezo wa kumueleza matatizo yetu ya ndani bila kumuonea aibu, ni tofauti kama angekuepo mwanamme.

Omar Khatib Omar mkaazi wa wingwi njuguni anasema suala la utekelezaji wa Sera ya Jinsia ni lazima kwani walipopata Sheha mwanamke maendeleo yalipatika.

Ilikua kuna baadhi ya Vijiji havina huduma ya Maji ila baada ya kuja Sheha mwanamke tumeondokana na shida hiyo, ambapo kabla ya yeye alikuepo mwaname anaeleza.

VIONGOZI WA SERIKALI
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya anaeleza kuwa, kiuhalisia mtendaji mkuu wa majukumu ya kazi ni mwanamke.

Anasema kama ofisi ya wilaya, watahakikisha kunakuwepo na usawa kwa kamati zote kuanzia ngazi ya shehia hadi wilaya.
ilaya.

ATHARI
Kutokushirikishwa kwa wanawake katika tasisi kunaweza kukapelekea kukosekana kwa fursa za kimaendeleo kwa baadhi ya makundi ya watu.

Mwanaisha Ali Masoud Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto Pemba anasema utekelezwaji wa Sera unahitajika kuanzia hata kwenye ngazi ya familia.

Tunataka kwamba kila alipo mwanamme na mwana mke awepo kwani shida za wanawake anazijua mwanamke,anaeleza.

VIONGOZI WA DINI
Sheikh Said Ahmed Mohamed kutoka Ofisi ya Mufti Pemba anasema, uislamu umemruhusu mwanamke kushiriki nafasi ya uongozi, anayoiweza kwa mujibu wa dini inavyoelekeza.

Mchungaji Yohana Ali Mfundo wa Machomane Chake chake, amefahamisha kuwa katika dini yao hakuzuiwa mwanamke asishiriki kwenye mamuzi, ilimradi afuate masharti yaliopo.

NYARAKA
Tamko la Jumuiya ya Maendeleo la nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) la mwaka 2005 na itifaki ya SADC ya Jinsia na maendeleo la mwaka 2008, ni kuhakikisha kuna usawa wa kijinsia katika ngazi zote za maamuzi.

Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020/2025 ni kuhakikisha inaimarisha usimamizi wa utendaji wa masuala mtambuka katika mamlaka za Serikali za mitaa kama usawa wa kijinsia.

Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na watoto Zanzibar ya mwaka 2024/2025 imebainisha kuwa, tafiti zinaonesha kuwa nchi zinazozingatia usawa wa kijinsia zimeweza kuimarika kiuchumi kwa kasi kuliko nchi ambazo hazizingatii usawa huo.

NINI KIFANYIKE?
Sheha wa Bopwe, anasema ni vyema na masheha wengine kuiga mfano wake kuhakikisha wanaweka uongozi sawa, kati ya wanawake na wanaume.

Andiko la: FATMA HAMAD, PEMBA
 
Back
Top Bottom