Wajuvi wa kiswahili, maana ya neno "bosheni" ni nini?

Wajuvi wa kiswahili, maana ya neno "bosheni" ni nini?

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
2,406
Reaction score
8,039
Nimeona likitumika mahali kadha wa kadha, asili ya ili neno bosheni ni nini? Na maana yake ni nini?
 
Mbona neno la kawaida sana haswa mikoa ya pwani.

Sisi bosheni ni kitu kama hakina uhalisi, kitu fake ...Mfano viatu vya special vile vya mabox sio og tunaita bosheni ..

Bosheni na geresha yanafanana kwa mbali .... yaani yanamaanisha kitu kipo pale ila sio halisia na hakina ubora ,yanatumika kweny mazingira tofauti.
 
Bosheni unaweza sema kitu feki lakini bado sio maana sahihi, boshen ni kitu kinachoundwa kianane na kitu halisia, kwa lengo maalum,

Kingereza kizuiri cha bosheni ni decoy au dummy.

Mfano unaweza sema. Wa Ukraine walipiga bosheni ya submarine ya Russia.
 
Back
Top Bottom