Wajuzi katika Kuzuia mitaro isizidi kuwa mabonde

Wajuzi katika Kuzuia mitaro isizidi kuwa mabonde

Jojo123

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2013
Posts
432
Reaction score
703
Wandugu JF,

Aisee kuna plot yangu nilinunua Salasala kilima Hewa miaka 7 iliyopita, kulikuwa kuzuri ila sasa naona baada ya ujenzi wa watu mbali mbali na kulingana na nature ya Hapa ni slope sana hivyo naona haka kamfereji kalikuwa Maghatibi mwa Plot yangu, na hakikunipa shaka mwanzoni ila ni kama vile kamekuja kuwa mtaro sasa, na unazidi chimbika kwenda chini sana mwanzoni nilichukulia kuwa ni mifereji ya kawaida kulingana na vilima vya huku nikaamini ni lazima kuwe kuna chanel za maji ya kutoka majumbani kwa watu yapite somewhere.

Sasa nimekuja kwenda site baada ya miaka mingi juzi nakuta ule mfereji umechimbika kwenda chini kwa ongezeko la mita moja na nusu. Halafu upana wake uneongezeka kwa cm50 kila upande.

Sasa shaka yangu kuu ni kwamba ile deepness yake ikipata erosion Ngema ita dondoka na mfejeji kuwa Bonde kubwa zaidi na kiwanja changu kuanza kuliwa zaidi.. Mwishowe nishindwe kuja kuumudu.

Je, njia gani rahisi ya kuzuia Mtaro huu usizidi kutanuka na ku chimbika zaidi?

Naomba kama kuna aliyefanikiwa kudhibiti Mtaro kwake atume picha hapa kwenye comment ili na mimi nijifunze mbinu tofauti na gharama kama naweza ambiwa gharama za kudhibiti mtaro kwa urefu wa wa mita45 upana mita3 na urefu kwenda chini ni mita 2. Natanguliza shukrani.

Asanteni

View attachment 1697220
 
Pia nakushauri utafute mafundi ujenzi wabobevu watakusaidia hii ishu
 
Pia nakushauri utafute mafundi ujenzi wabobevu watakusaidia hii ishu
Hilo neno pia inaonesha umesha toa ushauri kabla ya kuongezea huu wa kutafuta fundi.

Ila nimejaribu tafuta ushauri ulio tangulia sijauona.
 
ilo neno pia inaonesha umesha toa ushauri kabla ya kuongezea huu wa kutafuta fundi.

ila nimejaribu tafuta ushauri ulio tangulia sijauona.
😂😂😂Oya bro, Kiswahili hujanifundisha na nilipata mswaki
 
Sijapata ushauri mpaka leo.. Wajenzi mpo wapi??
 
Hapo solution ya kudumu ni kutengeneza gabions. Gabions inategemea na hali halisi ya mfereji kwahio km una picha piga nikuelekeze vizur baada ya kuona madhara Ni makubwa Kiasi gani kwenye kiwanja .gabions ni njia nzur yakulinda mmomonyoko wengine wanatumia mifuko ya cement iliyojazwa mchanga au udongo lakini ile ya kupanga mawe yakazungushiwa wiremesh ni Nzuri na yakudumu zaidi mara nyingi inawekwaga kwny kingo za mito Wakati wanajenga daraja
 
Jengea mtaro kama unavyoona wanajengae kwenye barabara kwa kutumia mawe na saruji pembeni na chini ila fundi ajenge vizuri Ili kuyachanel maji.Huo ujenzi uzingatie steps na scoring checks kupunguza Kasi ya maji

Sa sivyo tu funga gabions na matress
 
Nipe hiyo kazi nitazuia hayo mambo yanayo jitokeza.
 
Hapo solution ya kudumu ni kutengeneza gabions. Gabions inategemea na hali halisi ya mfereji kwahio km una picha piga nikuelekeze vizur baada ya kuona madhara Ni makubwa Kiasi gani kwenye kiwanja .gabions ni njia nzur yakulinda mmomonyoko wengine wanatumia mifuko ya cement iliyojazwa mchanga au udongo lakini ile ya kupanga mawe yakazungushiwa wiremesh ni Nzuri na yakudumu zaidi mara nyingi inawekwaga kwny kingo za mito Wakati wanajenga daraja
Mkuu unaonaje gharama za gabion ukilinganisha na kujengea mawe kwa cement? Na je mafundi wataalamu wa kufanya hii kazi wanapatikana wapi?
 
Back
Top Bottom