Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,156
Makabila mengi ya hapa Tanzania yana historia inayowatofautisha na Makabila mengine. Kwa muda sasa (takribani miaka mitano) nimekuwa nikifanya kazi hapa Morogoro chimbuko halisi la Waluguru. Kuna mengi nimeyaona kwao ambayo ki ukweli yanaacha maswali kwangu.
Mosi ni kuhusu elimu dunia. Ki ukweli vijana na wazazi wengi wenye asili ya kiluguru kwao elimu sio kipaumbele kwao. Ujio wa shule hizi za kata ni kama kwao imekuwa adhabu. Hapa ni kwa wote, wa kike na wa kiume.
Ningependa kufahamu, kwa nini mkoa huu mambo ya elimu hayapewi kipaumbele? Kuna sababu zozote za kihistoria zinazosababisha hili? Tunaambiwa mkoa huu hata matokeo yao kitaifa haufanyi vizuri! Naomba kufahamu.
Pili ni kuhusu ushirikina. Kwa muda niliokaa hapa nimeshuhudia mengi yanayoashiria vitendo vya kushabikia mambo ya kishirikina kwa wenyeji. Hii inahusisha matambiko, kujilinda (wenyewe wanaita), kwenda kwenda kwa waganga n. k. Hii pia haina vijana wala wazee, wote ngoma droo!!
Nalo lina link yoyote na historia ya mkoa huu? Kuna msitu maarufu sana unaitwa KOLELO maarufu sana kwa matambiko toka enzi hizo.
La mwisho ni kupenda starehe kupitiliza kuliko kazi. Wakaazi wa hapa kutwa kuchwa ni sherehe! Hadi mtoto anayetimiza mwaka anafanyiwa bethdei kwa kukodi mziki mnene na unapigwa tangu asubuhi hadi majogoo!! Hapo jumlisha visingeli na vigodoro vya kila mara mitaani vinavyotunyima usingizi
Mbona mikoa mingine haya hayapo kwa kiasi hicho? Nini chanzo cha haya yote hasa hapa mjini ukilinganisha na miji mingine