Wajuzi wa iphone msaada tafadhali

Wajuzi wa iphone msaada tafadhali

Paul S.S

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2009
Posts
6,407
Reaction score
3,260
Nina iphone 8 nimenunua kwa jamaa yangu yupo mbele na alisahau kufuta icloud acc, naomba msaada ufuatao

Iphone naitumia lakini ina Apple acc ya mshkaji.....kuna mambo siwezi fanya bila password ya icloud.
Inawezekana mshkaji akaingi kwenye acc yake ya icloud online kwenye itunes au website na kuiondoa acc yake kwenye hii simu au ni lazima anitumie password? (Hapa ndio ugumu uliopo kukubali kunitumia password yake)

Pili, kuna utundu wowote wa kudownload mp3 za akina shilole na kuzipeleka kwenye library ya Apple music player bila kutumia itunes?

Mwisho simu ina ios 13.5.1 nimejaribu kugoogle sijapata majibu muafaka......inawezekana ku jailbrake hio ios au nyingine za juu yake?

Natanguliza shukurani
 
Icloud account ndo kila kitu, chakufanya hapo mchek jamaa akutumie passwd then utoe otherwise umepipgwa na wajanja, kuhusu music tumia audimac au kama unataka utumie apple music uwe unatumia pc kuweka nyimbo kwa simu, ya mwsho kabisa ili kustream any time itabd uwe unalipia huduma ya applemusic
 
Anaweza kusign out tokea kwenye browser yake, alogin to iclooud aende kwenye list ya device achague iphone yako kisha asign out.

Kuhusu mp3 tafuta program inaitwa documents ipo app store developer ni readdle. Ina built in browser, file manager na download manager, kupitia hii app ingia browser (last time ilikuwa chini kulia) kisha download mp3 husika, itadownloadika humo humo ndani halafu kuna option ya kuhamisha kwenda kwenye main folder ili itambulike system wide na uione kwenye music player.

Maelezo zaidi hapa

Pia mkuu jifundishe kuweka Altstore ni store nyengine yenye apps ambazo Apple haziruhusu kwenye store yake, utapata apps ambazo zinakupa uhuru zaidi.
 
Thanx mkuu hatimaye nimefanikisha zoezi jamaa ame sign out na nimeweka icloud yangu sasa

So far App ya Documents ndio app yangu mama kwanye hiki kimeo changu pendwa
Nadownload na kusikilizia muziki yangu hapo hapo, ingawaje player yake sio pro kufanya playlist, inabidi nitengeneze folder mbali mbali na kuwa kama playlist zangu
Nadownload movies natumia xender kuhamishia kwenye galaxy yangu kisha kwenye memory card kisha naangalia kwenye tv

Bado sijapata music player decent, nimeweka vlc ambayo sio mbaya unaweza kuhamisha mp3 ulizodownload kwenye documents na kuzipeleka vlc, vlc wako vizuri kwenye movies

Documents inafungua RAR na ziped files, inafungua PDF files, ina VPN, inafungua epub book, ina play music/video, ina browser with downloader na ni file manager

Hii iphone 8 bado ipo ios 13.5.1 naona review nyingi wanasema ukiupdate kwenda ios 14 inakua inakula sana chaji, bado sijaamua

Ila haka kakimeo bana yaani kanajaa chaji chini ya lisaa limoja na kanajitahidi kukaa na chaji ila sio kama li backup phone langu galaxy tab a 2016, linachelewa kujaa ila linakaa sana na chaji

Kingine nime miss sana kusikiliza miziki nikiwa safarini na earphone
Hii haina tundu, na wireless earphone zake sina na bei imesimama

Mwisho App za ios zina mb nyingi sana na ukiangalia specifications za iphone unaona kama ndogo vile
Mfano RAM na MP za kamera lakini kwenye ufanisi aisee simu ipo very smooth hakuna kukwama kwama hata ufungue app zote
Kwenye kamera nako sio mchezo kulinganisha na MP kibao ya kwenye android
 
Back
Top Bottom