Wajuzi wa magari, ushauri wenu

Wajuzi wa magari, ushauri wenu

davetz28

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2017
Posts
543
Reaction score
624
Mimi ni mwanajukwaa mwenzenu japo si wa muda mrefu ila naheshimu Sana jukwaa hili kuwa ni mahali pa kupata maarifa mapya, ushauri kutoka kwa wabobezi.

Kwa kufupisha tu ni kwamba nimekuwa nikijiwekea akiba kidogo kidogo ili walau na mimi muda ukifika nipate japo ka usafiri ka kutembelea.
Sijawahi kumiliki usafiri japo Nina hamu sana ifike siku na mimi nimiliki chombo(gari)

Ombi langu kwenu ni ushauri wenu gari ipi ni nzuri hasa kwa mtu anayeanza kumiliki kwa mara ya kwanza? Binafsi napenda sana brand za Nissani japo wanasema zina gharama kubwa za uendeshaji.

Zipi gari imara,zinazodumu muda mrefu pia zinatumia mafuta kidogo na NI rahisi katika matengenezo yake?
Nategemea kupata milioni 13 kutokana na akiba yangu mwakani.

Je ipi salama,kuagiza au kununua hapa hapa kwa wanaouza gari zao?
ASANTE NI sana kwa muda wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chevrolet Trailblazer SUV itakufaa

BG832518_3ea8c3.jpg
 
Kwa bajeti ya m13 unaweza kuagiza gari Japan moja kwa moj bila shida...gari dogo..

Ili usaidiwe vizuri ungefafanua unataka gari la kuendesha mazingira ya lami au vumbi, kubebea mizigo au gaei la kupiga safari tu za hapa na pale...

Kama wewe ni Mpezi wa NISSAN kwa bajeti yako nakushauri chukua NISSAN TIIDA au Nissan Note zina cc 1500 na gharama zake ni za kawaida kiasi...kuhusu spea zipo japo ni bei kidogo na ukifunga ni mkataba ...Ukiagiza Japan uiweke mkononj moaka ianze kukusumbua vitu vikubwa kama suspension si chini ya miaka 5...naongea kwa kupitia uzoefu.

Kwa Upande wa TOYOTA nakushauri angalia IST old model, Run X au Allex japo hizi mbili zina bei kidogo au Raumu kwa mbaali... Hizi zote huja na injini za cc 1300 mpaka 1500....spea mpaka kwa mangi gengeni..

Haya magari niliyoyataja kutoka Nissan na Toyota ni magari rafiki sana kwa mtu anayemiliki gari kwa mara ya kwanza...ni model ngumu ukizitunza vizuri na zinaweza safari ndefu ndefu na ni rafiki kwa mafuta.

Angalizo.kwa sababu umesema ndiyo unataka kumiliki gari kwa mara ya kwanza , nakushauri ufikirie zaidi kuagiza Japan...utaepuka kero nyingi.Japo hapa hapa unaweza kubahatika kumvua mtu ila ni bahati nasibu na inapenda uwe na uzoefu na magari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
First timer, pesa ya hustling (so mafuta na service ni cincern), gari la kwendea job home church/mosque, misele kidogo, budget mil 13 max.

Kwa kuanza Brand yako ni Toyota, cha pili, agiza nje (Japan) cha tatu chagua Kati ya IST (uzuri wake ina high resale value), Runx/Allex, Premio/Allion, Vitz, Voltz (ila hii engine kubwa).

Kwepa Crown, Altezza, Brevis, Mark 2 na X, mbali na kwamba zina engine kubwa pia resale value yake sio nzuri baada ya mwaka tu.

Budget yako unaweza agiza gari za aina nyingi sana saaaana ila kua makini, kununua ni issue nyingine, na kumiliki noi topic nyingine.

Ushauri wangu tu huo, watakuja wengine na utachanganya na za kwako.
 
Kwa bajeti ya m13 unaweza kuagiza gari Japan moja kwa moj bila shida...gari dogo..

Ili usaidiwe vizuri ungefafanua unataka gari la kuendesha mazingira ya lami au vumbi, kubebea mizigo au gaei la kupiga safari tu za hapa na pale..
Mkuu nakuehukuru sana kwa uchambuzi makini. ASANTE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
First timer, pesa ya hustling (so mafuta na service ni cincern), gari la kwendea job home church/mosque, misele kidogo, budget mil 13 max.

Kwa kuanza Brand yako ni Toyota, cha pili, agiza nje (Japan) cha tatu chagua Kati ya IST (uzuri wake ina high resale value), Runx/Allex, Premio/Allion, Vitz, Voltz (ila hii engine kubwa)....
ASANTE mkuu. Nahitaji kwa ajili ya usafiri kurahisisha shughuli za biashara yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naomba ufafanuzi kidogo hapo kwenye alteza,mimi kwa uelewa wangu mdogo wa magari nilikuwa nadhani Alteza ipo kwenye category moja na akina premio.
Je ni nini disadvantages zake?
First timer, pesa ya hustling (so mafuta na service ni cincern), gari la kwendea job home church/mosque, misele kidogo, budget mil 13 max.

Kwa kuanza Brand yako ni Toyota, cha pili, agiza nje (Japan) cha tatu chagua Kati ya IST (uzuri wake ina high resale value), Runx/Allex, Premio/Allion, Vitz, Voltz (ila hii engine kubwa)...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ASANTE mkuu. Nahitaji kwa ajili ya usafiri kurahisisha shughuli za biashara yangu

Sent using Jamii Forums mobile app

Katika biashara utahitaji kubeba mzigo au? Yaani utakua unabeba mzigo kama ukubwa gani? Kama mzigo wa kawaida tu cheki izo.

Pia kumbuka kama utakua unazunguka zunguka Kariakoo, Town, mafuta na parking space, ni kigezo.
 
Mkuu naomba ufafanuzi kidogo hapo kwenye alteza,mimi kwa uelewa wangu mdogo wa magari nilikuwa nadhani Alteza ipo kwenye category moja na akina premio.
Je ni nini disadvantages zake?

Sent using Jamii Forums mobile app

Altezza ni nzuri as long as upo fresh kwenye wese.

Altezza kukaa stage moja na Premio sio fair coz Tezza ni sports oriented ila wakina Premio na Allion kiofisi/family zaidi.

Mfano tu mtu akishuka kwenye Altezza na Akishuka kwenye Premio unawachukuliaje? Utaona Altezza kijana wa mjini Premio mtu wa ofisini.

Pia Atezza resale value zinashuka ndio maana unakuta zinauzwa Mil 4-5 na nzima kabisa ila Premio ukiona Mil 7 ujuenamba C kurudi nyuma.
 
ASANTE mkuu. Nahitaji kwa ajili ya usafiri kurahisisha shughuli za biashara yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Premio is the best,Itakusaidia Shughuli za hapa na pale,Ina cc 1490 Hivyo ulaji wa mafuta si mkubwa..

Ni ngumu pia na imekaa Ki luxury na hata spea zake mjini zipo za kumwaga.

Ningeshauri Ist,Raum ama Runx ambazo nazo zina sifa nyingi nilizoainisha hapo juu ila Premio ni Luxury zaidi na kwa hyo pesa unaagiza kabisa direct kutoka Japan..

Good Luck

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni mwanajukwaa mwenzenu japo si wa muda mrefu ila naheshimu Sana jukwaa hili kuwa ni mahali pa kupata maarifa mapya, ushauri kutoka kwa wabobezi.

Kwa kufupisha tu ni kwamba nimekuwa nikijiwekea akiba kidogo kidogo ili walau na mimi muda ukifika nipate japo ka usafiri ka kutembelea.
Sijawahi kumiliki usafiri japo Nina hamu sana ifike siku na mimi nimiliki chombo(gari)....

Kama ndio gari ya kwanza unaweza kutafuta watu wakusaidie kuagiza Toyota IST nzuri kabisa. Itakufaa kwa hivyo vigezo vyako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, ebhu tuangalie gari hzi mbili chap chap... IST(1290&1498)na Premio F...nasisitiza premio F maana zipo za aina tatu...
Premio F ni 1498 cc, premio X 1790cc na premio G 1990 cc
Uzuri wa premio F ni kwamba unywaji wake wa mafuta ni mzuri mnoo ukilinganisha na gar nyingne ambazo ni luxury...

tukijaribu kulinganisha na IST yenye 1290, IST inakunywa vizuri kuliko premio F, lakini sasa tukija kwenye muonekano.... premio ipo vizuriii..
Sasa hapo ni wewe tuu kuchagua

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
ASANTE mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom