Wajuzi wa miamiala ya kibenki

Bitcoinbase

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2016
Posts
319
Reaction score
285
Habarini za jioni. Poleni na majukumu.

Naomba wataalamu wanisaidie kunipa mwanga juu ya hili lililonisibu.
Jioni hii nilikuwa nimeenda Kutoa pesa kwenye ATM,, baada ya kufanya transactions na kucomand withdrawal. Nikiwa nasubiri bahati mbaya ikapigwa Simu nikapokea nikasahau kuvuta pesa kwenye mashine, baadae nashtuka ndo zinaishia kurudi kwenye machine.

Na ile nikarudisha kadi tena kucheck balance Hamna ,, So naomba Kujua taratibu za kufuata ili ziweze kusoma kwenye account.. Nifanyaje, ?
 
Nenda ofisini kwa hio benki kesho watakusaidia. Ila jifunze kuweka vipaumbele (priorities). Hukupaswa kupokea simu mpaka umalizane na muamala. Pole sana
 
Nenda benki husika kawaeleze kuhusu hilo watakurudishia.

Hio hela ni kwamba ilishatoka kwenye akaunti hivyo salio lazima lipungue,kitendo cha hela kurudishwa sio kwamba inarudishwa kwenye akaunti ni ATM imehisi hakuna response hivyo imezirudisha ndani,kwahio hio hela yako wataikuta kwenye pesa za ATM ,ikiwa imezidi.

Wakiangalia na Kwenye Kamera kuthibitisha kwamba ni wewe watakurudishia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…