Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Nimesoma taarifa ya kuachiliwa kwa dhamana mahakamani aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Simuyu, Yahaya Nawanda kwa tuhuma zinazomkabili za ulawiti.
Zaidi soma: Dkt. Yahaya Nawanda apandishwa Kizimbani kwa Tuhuma za Ulawiti, aachiwa kwa dhamana
Kwa wajuzi wa sheria, Tuhuma za ubakaji na ulawiti zina dhamana?
Muda mrefu nimekuwa nikisikia haya ni mojawapo ya makosa yasiyo na dhamana.
Zaidi soma: Dkt. Yahaya Nawanda apandishwa Kizimbani kwa Tuhuma za Ulawiti, aachiwa kwa dhamana
Kwa wajuzi wa sheria, Tuhuma za ubakaji na ulawiti zina dhamana?
Muda mrefu nimekuwa nikisikia haya ni mojawapo ya makosa yasiyo na dhamana.
Kwa kuzingatia Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022. Kifungu Na. 148 (5)(a) kimeorodhesha makosa ambayo siyo ya dhamana yakiwemo;
- mauaji, uhaini, unyang'anyi wa kutumia silaha, au unajisi wa mtoto;
- Usafirishaji haramu wa madawa ya kulevya dhidi ya Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya;
- Kosa linalohusisha heroini, kokeini, opium etc;
- Makosa ya ugaidi kwa kuzingatia Sheria ya Kuzuia Ugaidi.
- Uhujumu uchumi kwa makosa kadhaa chini ya Sheria ya Utakatishaji Fedha Haramu.
- Usafirishaji haramu wa binadamu kwa kuzingatia Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu.
Kwa kuzingatia taarifa zilizopo ni kwamba mshtakiwa anatuhumiwa kwa kosa la kumwingilia kinyume na maumbile 'kumlawiti' kinyume na kifungu namba 154 (1) (a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16.
Hivyo ni sahihi kwa mahakama kumuachia kwa dhamana mshtakiwa.
Sababu nyingine ambazo zinaweza kupelekea mtuhumiwa kunyimwa dhamana ni pamoja na:
- Sababu za usalama wa mtuhumiwa mwenyewe akirudi uraiani
- Endapo mtuhumiwa alishawahi pewa dhamani na akaruka masharti ya dhamana.
- Endapo kosa linahusu pesa au mali yenye thamani zaidi ya milioni kumi unless mtu huyo atoe dhamani ya milioni kumi au mali yenye thamni hiyo.