Wakae pembeni kupisha uchunguzi

Waridi

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2008
Posts
1,025
Reaction score
172
Kufuatia kitendo cha kikatili cha kumteka, kumpiga na kumjeruhi vibaya sana Dr. Ulimboka, katika mazingira ya yeye na madaktari wenzake kudai haki, wafuatao wakae pembeni kupisha uchunguzi;
1. Waziri wa Afya (kwa kuwa ana dhamana ya wizara husika)
2. Afisa wa Ikulu, David (kufuatia tuhuma za kumpigia simu mwathirika)
3. Mkuu wa usalama wa Taifa (shuku ya umma kwamba idara anayoiongoza huenda inahusika)
4. ...
5. ...

Wabunge wetu komaeni na hili.
Tena itafaa kama uchunguzi utaendesha na vyombo vya kimataifa, maana hivi vya ndani huenda ndio hao hao wahusika.
 
Yan huyu david ana husika kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…