Wakala kutoridhika na Maandalizi ya Kituo cha kupigia Kura

Wakala kutoridhika na Maandalizi ya Kituo cha kupigia Kura

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
20201028_053829.jpg

Kifungu cha 52(2) cha Kanuni za Chaguzi za Taifa ( Uchaguzi wa Uraisi na Ubunge), 2020 kinaeleza kuwa:

Endapo wakala wa upigaji kura hatoridhika na maandalizi ya kituo cha upigaji kura atatakiwa kabla ya kuanza kupiga kura atoe malalamiko kwa msimamizi wa kituo au msimamizi msaidizi kupitia Fomu namba 14 kama ilivyoelezwa Katika Taratibu.

Kifungu 52(3) cha Taratibu hizi kinaongeza kuwa Msimamizi mkuu au msimamizi msaidizi wa kituo cha kupiga kura atatatua malalamiko hayo na kubainisha jinsi alivyotatua katika fomu No. 14
 
Upvote 2
Mizozo yote tuliyo nayo kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi kuto kufanyika vizuri una uhusiano mkubwa na maelezo uliyo toa. Kama tuhuma zote za kura za wizi niza kweli, kwanini mawakala wa upinzani hawaku fuata maelekezo hayo?
 
Jiongeze kwenye kufikiri. Zaidi robo tatu ya mawakala nchi nzima ama wamecheleweshwa kuingia kwenye vituo au kuzuiliwa kabisa. Hayo ya kuridhika na kituo yangefanyikaje?
 
Hawana lolote; ni kutafuta kisingizio tu. In fact mawakala wa mbowe wote walikuwa vituoni na walithibitisha kuwa kila kitu kilikuwa sawa; baada ya kuhesabu kura ndipo wakapata msituko wa moyo na kutafuta sababu nyingine.
 
Mizozo yote tuliyo nayo kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi kuto kufanyika vizuri una uhusiano mkubwa na maelezo uliyo toa. Kama tuhuma zote za kura za wizi niza kweli, kwanini mawakala wa upinzani hawaku fuata maelekezo hayo?
Yaliyopita ni histori chungu, yatabaki kuwa rejea kwa vizazi vyetu. Walio fanikisha uovu huu, we ikiwemo, mnajishauwa huku ukweli mkiujua. Hao mawakala wengi waliziuwa kuingia kwenye vyumba. Waliodiriki kuelezea malalamiko walituhumiwa kuleta fujo na kuishia mikononi mwa polisi, lakini Leo unajidai kuwalaumu kutojaza fomu za malalamiko.
 
Yaliyopita ni histori chungu, yatabaki kuwa rejea kwa vizazi vyetu. Walio fanikisha uovu huu, we ikiwemo, mnajishauwa huku ukweli mkiujua. Hao mawakala wengi waliziuwa kuingia kwenye vyumba. Waliodiriki kuelezea malalamiko walituhumiwa kuleta fujo na kuishia mikononi mwa polisi, lakini Leo unajidai kuwalaumu kutojaza fomu
Nafikiri hoja yako ingekuwa uwezekano wa kuwepo njia ya kupinga matokeo mahakamani kama njia ya kudumisha demokrasia. Hilo linge wezekana, na ushahidi unge kuwepo basi tungekuwa tuna ongea lugha moja
 
"Msimamizi mkuu au msimamizi msaidizi wa kituo cha kupiga kura."
Yaani umekaa na kuamini hao watu wako "neutral" kabisa!?
 
"...Msimamizi mkuu au msimamizi msaidizi wa kituo cha kupiga kura..."
Yaani umekaa na kuamini hao watu wako "neutral" kabisa!?
Kamanda mkuu aliye jiandaa kwa maandamano, una amini kabisa kwamba Rais Magufuli haku chaguliwa na watanzania walio wengi. Wala huoni umuhimu wa kuwa na njia za kistaarabu za kutatua changamoto kama za uchaguzi
 
Jiongeze kwenye kufikiri. Zaidi robo tatu ya mawakala nchi nzima ama wamecheleweshwa kuingia kwenye vituo au kuzuiliwa kabisa. Hayo ya kuridhika na kituo yangefanyikaje?
Si kuna utaratibu wa kufata endapo wakala kazuiliwa au kacheleweshwa kuingia kwenye kituo cha kupigia kura?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom