Wakala Morogoro avamiwa na kuporwa Milion 2 na vibaka

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Mfanyabiashara wa Miamala ya Kifedha alinayefahamika kwa jina la Method Asheri Mkazi wa Mtaa wa Majengo Mapya Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro amevamiwa na Watu wasiojulikana Kisha kuporwa begi lake ambalo lilikuwa lina Fedha zaidi ya Shilingi Milioni 2 ,Simu na Vifaa vyote vinavyotumika katika kufanya Miamala.

Akizungunza na AyoTV Method anasema tukio hilo limetokea majira ya saa Nne na nusu usiku ambapo alikuwa kwenye Pikipiki na Mwajiri wake kabla ya kuingia ndani gafla Vijana Wanne wakiwa na Mapanga wakawavamia na kuwajeruhi Kisha kutokomea kusikojulikana.

Soma pia: Waziri Ulega asitisha bunge na kwenda kutizama uharibifu wa miundombinu Morogoro

Your browser is not able to display this video.


Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Majengo Mapya lilikotokea tukio hilo Kassim Mng’ande amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kwa sasa Ulinzi Shirikishi unaendelea ili kuimarisha ulinzi.

Chanzo: Millard Ayo tv
 
Milioni 2 ni matumizi ya muda mfupi mno,pole Yao vibaka.

Huyo wakala Mungu ampe wepesi
 
Morogoro Nako Kwa Moto Sana
 Mawakala Wanaporwa Sana Mpaka Kuuwawa
 
Ndoto ya chura a.k.a Dalali imetikia watanganyika kuteseka kwao.
Na Bado mpk mjitambue yy wala hana time na nyie.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Ndoto ya chura a.k.a Dalali imetikia watanganyika kuteseka kwao.
Na Bado mpk mjitambue yy wala hana time na nyie.
Kazi ni kipimo cha utu
Peleka usenge wako huko, km mmeshindwa siasa za majukwaani msidandie kila kitu. Tafuteni kazi nyingine ya kufanya
 
Nisivyoamini viumbe,
bwamdogo anaweza kula deal na vibaka wampore wakagawane.
Hasara kwa mwenye mtaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…