Wakala wa Air Tanzania ~ Comoro wakutana na balozi Yakub

Wakala wa Air Tanzania ~ Comoro wakutana na balozi Yakub

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Said Othman Yakub amekutana na kufanya mazungumzo na wakala rasmi wa Air Tanzania hapa Comoro ComAir waliowakilishwa na Ndugu Kamarouddine Waziri Zamane pamoja na Maafisa wa ATCL walioko Comoro Bi. Esther J Mahiga na Bw. Boudra Fahit.

Mazungumzo yao yalijikita katika masuala mbali mbali ya operesheni za Air Tanzania hapa Comoro na namna ubalozi kama wawakilishi rasmi wa Serikali wanavyoweza kusaidia. Pia, Balozi Yakubu alitumia fursa hiyo kuwapongeza kwa kujali wateja wa Comoro ambapo hivi sasa ATCL wanafanya safari tatu kwa wiki baina ya Dar es salaam na Moroni na ndege ya nne ya mizigo pekee inatarajiwa kuanza safari zake tarehe 13 Septemba, 2024.

Jitahada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuifungua Tanzania kibiashara ni pamoja na uwezeshaji mkubwa anaoufanya katika shirika la ATCL.

IMG-20240829-WA0013.jpg
IMG-20240829-WA0012.jpg
IMG-20240829-WA0018.jpg


Pia soma:Watanzania Waishio Comoro Wakutana na Balozi Yakubu
 

Attachments

  • IMG-20240829-WA0017.jpg
    IMG-20240829-WA0017.jpg
    97 KB · Views: 4
  • IMG-20240829-WA0016.jpg
    IMG-20240829-WA0016.jpg
    114.4 KB · Views: 5
  • IMG-20240829-WA0014.jpg
    IMG-20240829-WA0014.jpg
    102.2 KB · Views: 6
  • IMG-20240829-WA0015.jpg
    IMG-20240829-WA0015.jpg
    81.5 KB · Views: 4
  • IMG-20240829-WA0011.jpg
    IMG-20240829-WA0011.jpg
    104 KB · Views: 7
Back
Top Bottom