Wakala wa bank CRDB, NMB

Wakala wa bank CRDB, NMB

Ashirafu mpaleje

New Member
Joined
May 23, 2021
Posts
1
Reaction score
1
Wanajamii naombeni mnisaidie taratibu na kanuni za kuzifata ili kupata authorization za kuwa wakala wa bank tajwa hapo juu.

Nisaidieni tafadhali.
 
akala wa bank tajwa hapo juu!!! Nisaidieni tafadhali!!!
Anzia kwenye ukurasa wa CRDB, ili kupata taarifa.

Vigezo na Mahitaji​

  • Lazima uwe mfanyabiashara binafsi au kampuni
  • Ni lazima uwe na biashara inayoendelea, inayoendeshwa kihalali na uwe na leseni ya biashara
  • Uwe unafanya kazi katika eneo la biashara la kudumu lenye miundombinu inayofaa, uwezo wa kifedha na rasilimali watu ili kuweza kutoa huduma kwa ufanisi na usalama.
  • Mtu/Biashara lazima isiwe na rekodi mbaya ya madeni kwenye benki au taasisi yoyote ya kifedha kwa muda wote wa makubaliano ya uwakala
  • Mtu/Biashara haitakiwi kuendesha huduma ya Benki kama shughuli yake pekee na lazima uwe na kitambulisho cha NIDA
  • Mtaji wa chini kabisa ni Tsh Milioni 2 na ada ya maombi ya uwakala ni Tsh 350,000 ambayo haiwezi kurejeshwa mara wakala atakapoidhinishwa na kusaini makubaliano.
Code:
https://crdbbank.co.tz/sw/product/business/accounts/19
 
Back
Top Bottom