Wakala wa kupinga sensa akamatwa Singida akigawa vipeperushi vya kugomea sensa kwa Waislam

Wakala wa kupinga sensa akamatwa Singida akigawa vipeperushi vya kugomea sensa kwa Waislam

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
Ustadhi mmoja katika mkoa wa Singida amekutwa na vipeperushi zaidi ya 53 akivigawa kwa raia wanaoaminika ni wa kiislam ili kuwahamasisha kutojiandikisha katika zoezi la sensa ya watu na makazi mapaka vitu vifuatavyo vitakapowekwa katika dodoso hilo.

1. Kipengere cha dini

2. Uwiano wa mawakala kati ya wakristo na waislam

Source Clauds Fm habari
 
Aburuzwe mahakamani huyo kwa kosa la jinai na uhaini
 
DUUH!!!Ama kweli ni bora kunyimwa vyote kuliko kukosa hekima na busara!!!
 
Mwe! Nchi ina vituko hii, wadau wenzangu na sisi tugomee sensa hadi kipengele cha WANYWAJI kiwekwe,kwani sisi ndo walipaji wakubwa wa kodi inayosaidia bajeti ya nchi hii!
 
Jamani, mjumbe hauawi. Katumwa tu huyo. Na huwezi kuua mgomba kwa kuukata jani.
 
Kwa kweli hakuna uhusiano wowote kati ya sensa na dini. Nijuavyo serikali ya Tanzania haiongozwi kwa misingi ya dini yoyote. Hivyo kwa kuwa serikali ndiye mdau na mtumiaji mkuu wa taarifa za sensa haihitaji kujua waislamu au wasio waislamu ni wangapi ili iweze kupanga mipango kwa watu wake. Nionavyo kama madhehebu za dini zinahitaji kujua idadi ya waumini wao, waiombe Ofisi ya Taifa ya Takwimu iwasaidie utaalam wa namna ya kuwajua waumini wao bila ghalama kubwa na kupigizana kelele na serikali.
 
Ndiyo maana tulisema hii kazi ingefanywa na walimu.Watu wenye ethics zao.
 
nawashauri ndugu zangu waislam washiriki sensa ya serikali ikiisha waitishe ya kwao wenyewe wajihesabu kwa gharama zao wenyewe.wasitusumbue.kwani kipindi hiki ndo wameona umuhimu wa kujua idadi yao.they could have done it some years ago.
 
Hivi unajua ni upuuzi sana....jambo linalogharimu maBilioni ya shilingi lenye manufaa kwa watu karibia milioni 45, yaani vijitu vichache tu na interest zao wanozijua wao kwa kivuli cha uDini wanataka kuvuruga! Kama wanaopinga kwa nini wasikatae kuhesabiwa wao na wake zao wakaacha wengine waamue wenyewe! Kampeni ya nini na vipeperushi kibao!? Na kama ni msingi/msimamo wa dini...kwa nini waIslam wengine wanataka kuhesabiwa!?
 
HUYO KIDAGAA WAANZE KUKAMATA MAPAPA YALIYO MTUMA ili kukata mizizi
 
Ustadhi mmoja katika mkoa wa Singida amekutwa na vipeperushi zaidi ya 53 akivigawa kwa raia wanaoaminika ni wa kiislam ili kuwahamasisha kutojiandikisha katika zoezi la sensa ya watu na makazi mapaka vitu vifuatavyo vitakapowekwa katika dodoso hilo.

1. Kipengere cha dini

2. Uwiano wa mawakala kati ya wakristo na waislam

Source Clauds Fm habari

Duniani kote kuna mambo kadhaa yanayofanyika katika jumuiya ya waislamu na ambayo yanatoa reflection isiyo nzuri juu ya dini ya kiislamu katika jamii kwa ujumla. Hili ni mojawapo.
 
Kila mtu ana haki yake ya kuprotest kwa mambo anayoyaona kwake si mazuri.... nilivyosikia ni kwamba kwenye dodoso za sensa kuna kipengele cha kuhesabu misikiti na makanisa ... hapo ndipo suala la dini linapoibuka kwa nini uhesabu misikiti na makanisa kujua yapo mangapi wakati hutaki kujua waumini wa misikiti hiyo na makanisa hayo wapo wangapi.... nini siri hasa ya kujua misikiti ipo mingapi na makanisa yapo mangapi?..... watu wanaplani zao za kujua je malengo yao wamefikiwa kwa ajili ya kujenga misikiti au makanisa... kama agenda zao zilivyo...
 
Back
Top Bottom