Wakala wa mbegu ASA wamesababishia wakulima wa alizeti hasara kwa mbegu yao ya STANDARD

Mandison

Senior Member
Joined
Mar 10, 2017
Posts
191
Reaction score
110
Wakala wa mbegu Tanzania (ASA) mjitafakari sana! Mliwaaminisha watanzania kuwa mbegu yenu ya alizeti mnayoiita STANDARD ni mbegu bora kumbe ni mbegu ya hovyo kabisa! Ni bora mngeacha wakulima waendelee na mbegu za kienyeji ambazo ni nzuri na zinatoa mazao mengi kuliko huu upuuzi mlioaminisha wakulima kuwa ni mbegu bora na kuwatumbukiza katika hasara isiyo na mfano wake!
Cha kusikitisha ASA wameanzisha group la WhatsApp lakini wameamua kukaa kimya kwa kila changamoto wanayoletewa na wakulima wa alizeti!
 
Ulipata changamoto gani?
Binafsi zilikuwa ndefu sana na hasikubeba .
Zilikuwa ndogo ndogo.
Sababu za kutobeba.
1 mvua ilikata kipindi cha ubebaji.
2 kupuuzia mbolea.
Huo ni utafuti wangu binafsi.

Pia hazina mapepe mengi
Zina mafuta wastani wa 3kg /1lt
 
Mvua ilikuwepo ya kutosha na mbolea niliweka. Mazao ni kidogo mno japo zilionesha kustawi sana
 
Mvua ilikuwepo ya kutosha na mbolea niliweka. Mazao ni kidogo mno japo zilionesha kustawi sana
Ni kweli mkuu hawa ASA wamezingua sana mwaka huu. Ngoja tutafute mbegu zetu asilia
 
Ni kweli mimi nimelima alizeti imerufuka zaidi ya mita tatu halafu inazaa tochi nyingi sana.Mbegu zao siyo nzuri zinaleta hadara kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…