wembeee
JF-Expert Member
- Jan 16, 2015
- 2,708
- 1,353
.
Amesema hata kama Liverpool watakuwa tayari kumlipa Sterling paundi 900,000 kwa wiki bado hatosaini mchezaji huyo.
Amesema Sterling anataka kuondoka timu hiyo.
Na atajiunga na moja kati ya wapinzani wa Liverpool kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (Chesea au Manchester City).
Asema hajali kuhusu Liverpool wanawaza au kusema nini bali Sterling anaondoka.
Amuita Jamie Carragher ni "mjinga".
Kesho ijumaa Sterling atakutana na afisa mtendaji mkuu wa Liverpool na kuzungumza kwa mara ya mwisho kuhusu mkataba mpya.
Manchester United nao wamejaribu kumuulizia wakaambiwa hauzwi.
Raheem Sterling hatosaini mkataba mpya Liverpool hata kama klabu hiyo itampa ofa ya paundi laki tisa kwa wiki, amesema wakala Aidy Ward wa mchezaji huyo.
Ward anatarajia kuwa Sterling anaweza kuhamia Chelsea au Manchester City na kuzitupilia mbali Barcelona, Real Madrid na Bayern Munich.
Ward pia amewajibu vikali wachezaji wa zamani na wachambuzi wa mpira waliomkosoa kinda huyo mwenye miaka 20, huku akimtaja wazi Jamie Carragher ni "mpumbavu" au "mjinga".
Ward asubuhi ya leo huko Uingereza ameiamba London Evening Standard kuwa mchezaji huyo hatosaini mkataba mpya hata kama akipewa mshahara wa karibia paundi milioni 1 kwa wiki na anaweza kurudi London kuichezea Chelsea.
Amesema hajali kuhusu Liverpool au sifa yao na amepuuzia maneno yaliosemwa na wachezaji wa zamani wa Liverpool kwa kusema kuwa hayahusiani. Pia amemuita Jamie Carragher ni "mjinga".
Ward amesema;
"Sijali kuhusu mahusiano ya klabu na hali ilivyo kwenye klabu. Sijali. Hakika hatosaini. Hatosaini hata kwa paundi 700,000, 800,000 au 900,000 kwa wiki. Hasaini. Kazi yangu ni kuhakikisha nafanya kilicho bora kabisa na wao (wateja wake yaani wachezaji). Kama watu wanasema mimi ni mbovu kwenye kazi yangu au wanashauriwa vibaya, wala haijalishi (haihusu)".
Ward amemjibu vikali mmoja kati ya wakongwe wa Liverpool, Jamie Carragher. Amesema;
"Carragher ni mjinga. Kila mtu anajua hili. Ukosoaji wowote kutoka kwa wachambuzi wa sasa au wachezaji wa zamani wa Liverpool hakuna unaonigusa. Hakuna uhusiano.
Aliongeza;
"Sina wasiwasi. Mwenye wasiwasi anafanya maamuzi bila kujua nini kitatokea. Kila timu ya ligi kuu itamtaka".
Manchester United ambao ni wapinzani wakubwa wa Liverpool, leo imefichuliwa kuwa walijaribu kumtaka mchezaji huyo lakini wakajibiwa hauzwi.
Hakuna mchezaji yeyote baina ya timu hizi mbili aliewahi kutoka timu moja wapo na kuhamia kwa mpinzani mwingine tokea mwaka 1964 ambapo mchezaji Phil Chisnall alitoka Man United na kuhamia Liverpool.