Wakala wa Tigo Pesa kuwa makini na huu utapeli

Heavy Weight

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2014
Posts
888
Reaction score
885
Juzi kwa mara ya pili nimepigiwa simu na mtu anaejidai kuwa ni mhudumu wa tigo pesa toka makao makuu, akidai kuwa anataka kunisaidia kuongeza kamisheni yangu. Ambayo anasema ilikatwa kimakosa mwezi wa nne na wa tano. Kwa kawaida tigo wamekuwa walitutumia message kuepukana na watu wanaopiga simu na kujidai ni watu wa tigo wanataka kurekebisha kamisheni kumbe matapeli. Tigo hawawezi kukupigia simu na hata kama ukiwa na shida utawasiliana na wakala wako mkuu wa eneo ulilopo.

Swali la kujiuliza ni, Hawa matapeli wanakujua vipi na namba zako wanazitoa wapi? Huku wakitaja hadi jina lako la uwakala?

Jibu ni kwamba siku unapoenda kwa wakala wako mkuu kuingiza fedha (flot) kwenye line yako ya uwakala kuna karatasi unapewa ujaze taarifa zako, kwenye hiyo karatasi utaandika namba yako, kiasi cha fedha pamoja na jina lako la uwakala, vile vile hiyo karatasi (form) hauijazi peke yako kuna wengine wengi wanaitumia kujaza taarifa zao, na inawekwa juu ya meza ambayo kila mtu anaiona. Hivyo basi hao matapeli wanaweza kufika ofisini kwa huyo wakala mkuu kwa lengo la wao pia kupata huduma mbali mbali kisha wanachukua taharifa zako.

Wakishachukua taharifa zako (ulizojaza kwenye iyo form) wanakupigia simu na kujitambulisha kama mawakala kutoka tigo makao makuu. Wanaomba namba yako ya pembeni mbali na hiyo ya uwakala ambayo unatumia kwa mawasiliano ya kawaida, hata ukisema huna simu wanakwambia azima hata ya mtu yeyote wa jirani wakupigie kupitia hiyo namba.

Ukishampa namba anakupigia kisha anasema chukua simu yako ya tigo pesa kisha fuata maelezo anayokupa. Anakuambia uingie menyu ya tigo pesa na ukiendelea na kufuata maelekezo yake utajikuta umemtumia hela hivyo basi utakuwa umetapeliwa. Huwa wanaangalia watu wanaoingiza hela nyingi kwakuwa mimi mara ya kwanza waliponipigia asubuhi yake niliingiza million mbili na nusu jioni wakanipigia.

Juzi aliponipigia akaniomba namba ya pembeni nkamwambia sina akaomba namba ya mtu yeyote wa karibu yangu ili anpigie. Nilipompa akanipigia akasema niingie menu ya tigo pesa nkamuuliza maswali kwaajili ya nini akakata simu.

KUWA MAKINI NI MATAPELI
 
Wacha kuharibu dili za watu wewe😉😉
 
Mjini shule. Asante kwa taarifa.
 
Na pia wanao weka karatasi ya kutolea hela "(Namba ya Wakala " Agent code ~) nje hakikishani mnaangalia kama namba iko sahihi ,siku hizi unaweza ukakauta karatasi namba ya Wakala ni tofauti kabisa Mteja akitoa hela inaenda kwa matapeli, utalipa kwa sababu uzembe chunguza angalia ofisi yako vizuri kuweni makini [emoji1][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mimi natumia zimu special kwa kurusha Vocha zinatoka tigo hizo simu huwezi kupigiwa wala kupiga hiyo ni special kwa miamala tu ,au utume message

Kila wakipiga unaambiwa number bize , mpaka wananitumiaga text za matusi [emoji1][emoji1][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Jamaa wanafanya uhuni sana wazitafte kwa uhalali
 
Hapo umewaweza sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…