Wakala wa Vipimo nchini (WMA) imewaonya wafanyabiashara nchini watakao fungasha bidhaa zao kwa mtindo wa Lumbesa watakumbana na adhabu kali ya kifungo cha miaka mitatu hadi saba jela pamoja na kulipa faini.
Wafanyabiashara hao pia wametakiwa kutumia mizani katika kupima bidhaa zao wanazouza na sio kutumia vipimo vya kukadiria kwani vinawapunja wakulima na hivyo serikali kukosa mapato.