Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
In short equalizer zote ni kali yaani 1-3Maskini msichana Alina, mwili wake ulitumikishwa vibaya sana kingono...
Bahati mbaya hakuwa na wa kumsimulia anayopitia, kwa sababu wahusika walikuwa na nguvu kwenye kila idara..
Kuanzia kifedha, kisilaha, hadi kimakundi, ni Russian Mafian Mobb, wauza madawa, na human trafficking...
Alina alilala na wanaume kama walivyotaka wao, na pesa alipewa ya kubadilishia nguo tu, zote wakaziweka kwenye mifuko yao..
Kwao Alina ni bidhaa kama bidhaa zingine, anaenda sokoni, ananunuliwa, faida ni ya kwao..
Hadi alipokutana na Robert McCall,wakaunda urafiki, akawa sehemu ya faraja yake kwa mchana..
Ikafika siku ambayo Robert McCall alipoambiwa Alina yupo hoi hospitali, kwa sababu ya kupigwa kama mwizi..
Akafunga safari hadi kwa wamiliki wa msichana Alina, akataka kuijua thamani yake, ili amnunue awe huru..
Kwake tukio la kumpiga Alina, lilimgusa kama Baba, au mwanaume yoyote anaejali kuhusu mwanamke..
Walikataa, walimcheka, na mwisho wakataka wafanye vyote viwili, wachukue pesa, na wasimuachie huru msichana Alina..
Na hapo ndipo walipokosea, wao ni Mafia ndio, na ni watu wanaoogopeka, lakini huyu Robert McCall ni nani?..
Ni former Marine and retired DIA officer, binadamu anaejua akipiga wapi anaua, na wapi akigusa, utamtaja mzazi wako..
Wao walijua wamesimama mbele ya mtu mchovu, mpole, asiejiweza hata kidogo..
Lakini hii ilikuwa ndio siku yao ya mwisho kuliona jua la alfajiri, huyu Robert McCall ni Denzel Washington tunaemjua..
Akawawekea stop watch, akawaambia ndani ya sekunde 16, kila mtu atajuta alichochagua, sekunde 16 tu..