Tipstipstor
JF-Expert Member
- Nov 29, 2021
- 1,528
- 3,352
Ahlan wa sahlan
Wakamaria aka (gamblers) ,ni miongoni mwa watu wasio na furaha hapa ulimwenguni. Mwanadam ameumbwa akiwa na sifa ya kupenda umiliki na anachukia sana kitu ambacho amekimiliki kikimtoka.
Uchezaji wa kamari ni jambo ambalo limeharibu maisha ya watu wengi sana hapa duniani.Kamari imepelekea matajiri kufilisika, biashara kuharibika, mitaji kupotea na mbaya zaidi ni uharibifu wa familia nikimaanisha mchezaji kamari na watu wake wa karibu wanaomzunguka.
Watu wengi sana wanaocheza kamari huwa wanaficha uhalisia wa tatizo walilonalo yaani Uraibu wa kamari ( gambling addiction) , ni ngumu sana kumtambua mraibu wa kamari (gambling addict) kwasababu hakuna ishara yoyote ya nje ambayo inamuonesha kuwa huyu mtu ni mraibu wa kamari. Tofauti na uraibu mwingine ,kama ulevi wa pombe, ulevi wa madawa ya kulevya n.k
Kwavile hakuna ishara yoyote ambayo mtu anaweza kumtambua mkamaria, wakamaria wengi hulificha tatizo hili kiasi kwamba hata mke wake anaelala nae kitanda kimoja hawezi kujua kuwa mumewe ni mraibu wa kamari.
Binadamu anachukia sana kupoteza, iwe pesa,nyumba,mke,watoto n.k hakuna nwanadamu atakaesema kuwa anapata furaha pindi anapopoteza. Mraibu wa kamari huwa anapitia nyakati ngumu sana za msongo wa mawazo, mood swings...yaani kuna muda akishinda anajihisi afadhali na muda mwingi anapopoteza hali yake huwa ni mbaya sana. Huwa hana furaha kabisa na anatamani kuwa ifike siku aachane na uchezaji wa kamari ila kuna nguvu inamrudisha ikimpa matumaini mapya kuwa anaweza kurudisha kile alichopoteza na hapa ndipo anapoendelea kupoteza.
Ushauri wangu kwa vijana wenzangu ni kuwa tujiepushe sana na uchezaji wa kamari. Kamari imeharibu maisha ya wagu wengi sana hapa duniani na kuna takwimu zinazoonesha kuwa kila dakika moja kuna mtu anajiua kutokana na uraibu wa kucheza kamari.