Wakati abiria wa ajali za ndege wanalipwa mabilioni, Serikali iangalie abiria wa ajali za magari

DodomaTZ

Member
Joined
May 20, 2022
Posts
84
Reaction score
118
Kwanza nawapa pole wote walioathirika na ajali ya ndege na Precision Air kule Bukoba, pia napongeza walichofanya wale wavuvi katika uokoaji .

Lakini moja ya kitu ambacho kimenishangaza ni jinsi viongozi wa kisiasa walivyoikomalia suala hili katika sura nyingine ya bima.

Naelewa ajali za ndege ni nadra lakini hiyo haimaanishi mamlaka zitoe kipaumbele kwenye bima za ndege na kusahau zile za magari tena ambazo zinaua watu wengi kila siku.

Serikali na mamlaka za bima ziwe fair, nashauri elimu itolewe kwa wingi kuhusu bima za magari kwa kuwa wengi ambao wana uelewa hiyo kitu ni madereva na wamiliki wa vyombo.

Kitu kifanyike, abiria wengi wanakufa, wanaumia, wanapata ulemavu na athari nyingine nyingi lakini hawajui haki zao kutoka kwenye mamlaka za bima.
 
kabisa, huku barabarani ajali ni kitu cha kawaida saana lakini hakuna anayetilia maanani, mkazo ulipaswa kuwekwa ili watu wawe wanalipwa kuanzia majeruhi na wanaokufa, Mabus yoote yanapaswa kuwa na bima inayoweza kucover abiria incase na wenye mabus nao wabebeshwe mzigo fulani wa gharama fulani fulani ili nao wawe serious na biashara yao..
 
Mabus yoote yanapaswa kuwa na bima inayoweza kucover abiria incase na wenye mabus nao wabebeshwe mzigo fulani wa gharama fulani fulani ili nao wawe serious na biashara yao..
Nakazia
Zaidi ni iwe kwa vyombo vyote vya usafiri, hasa vya moto!
 
Hua nashangaa kweli askari barabarani wana juhudi kweli kuangalia bima kwenye magari ila pata ajali kwenye hayo magari kama hutajiuguza mwenyewe na hata mia hupati unajiuliza sasa hizi mbwembwe zote za nini sasa kama sisi wahusika hatulipwi hata mia mbovu
 
Itakuwa zile bima niza chombo cha moto tu labda
 
kabisa, huku barabarani ajali ni kitu cha kawaida saana lakini hakuna anayetilia maanani, mkazo ulipaswa kuwekwa ili watu wawe wanalipwa kuanzia majeruhi na wanaokufa, Mabus yoote yanapaswa kuwa na bima inayoweza kucover abiria incase na wenye mabus nao wabebeshwe mzigo fulani wa gharama fulani fulani ili nao wawe serious na biashara yao..
... na wa bajaji? Hutazungumzia hili kwa sababu una bajaji zinasanya.
 
Hua nashangaa kweli askari barabarani wana juhudi kweli kuangalia bima kwenye magari ila pata ajali kwenye hayo magari kama hutajiuguza mwenyewe na hata mia hupati unajiuliza sasa hizi mbwembwe zote za nini sasa kama sisi wahusika hatulipwi hata mia mbovu
Ukishapata ajali tu unatakiwa umkabidhi kazi wakili yeye ndio hufuatilia kila hatua hadi unalipwa unachostahili
 
Wengi hawajui kwamba baada ya ajali unatakiwa umpe kazi wakili yeye ndio atafuatilia mpaka unapata haki yako,
Ukienda kufauatilua mwenyewe wanakuzungushaaaa weeeee, si wanajua hujui sheria, sasa mpe tu mwanasheria kazi kisha tulia ule neema
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Kwanza nawapa pole wote walioathirika na ajali ya ndege na Precision Air kule Bukoba, pia napongeza walichofanya wale wavuvi katika uokoaji .

Lakini moja ya kitu ambacho kimenishangaza ni jinsi viongozi wa kisiasa walivyoikomalia suala hili katika sura nyingine ya bima.

Naelewa ajali za ndege ni nadra lakini hiyo haimaanishi mamlaka zitoe kipaumbele kwenye bima za ndege na kusahau zile za magari tena ambazo zinaua watu wengi kila siku.

Serikali na mamlaka za bima ziwe fair, nashauri elimu itolewe kwa wingi kuhusu bima za magari kwa kuwa wengi ambao wana uelewa hiyo kitu ni madereva na wamiliki wa vyombo.

Kitu kifanyike, abiria wengi wanakufa, wanaumia, wanapata ulemavu na athari nyingine nyingi lakini hawajui haki zao kutoka kwenye mamlaka za bima.
Bima za ndege ni Kimataifa
 
Mbona Sheria za bima ziko wazi na sawa kwa vyombo vyote? Ni lazima gari au pikipiki iwe na bima, si tu kukilinda chombo, hata waathirika wengine. Sasa je tunafuatilia ulipaji wa bima, na pia madai pale tunapokumbwa na janga la ajali?
Uelewa finyu wa haya masuala, rushwa na njia za mkato, zinatuponza sisi wenyewe yanapotukuta majanga.
 
Hua nashangaa kweli askari barabarani wana juhudi kweli kuangalia bima kwenye magari ila pata ajali kwenye hayo magari kama hutajiuguza mwenyewe na hata mia hupati unajiuliza sasa hizi mbwembwe zote za nini sasa kama sisi wahusika hatulipwi hata mia mbovu
Uelewa wa wahanga juu ya bima ni finyu. Umepata ajali, cha mwanzoni baada ya kuhakikisha matibabu ya awali ni kupata taarifa za bima za aliyekuumiza. Na ufuatilie ili ulipwe bila ya kuchoka, maana utakatishwa tamaa kwa mlolongo wa hatua za kuchukua n.k. na kila uendapo iwe polisi au mahakamani ni rushwa mbele, si ndio tunajiendekeza kuwa hakuna litakalofanyika bila ya rushwa. Sasa likikupata ndio utaona ubaya wa rushwa tunayoiendekeza!
 
Kitu kikubwa kwenye bima za ajali ya magari ni kuwa na tiketi. Tiketi ndio msingi wa madainya bima. Mabasi mengi siku hizi ya comprensive hivyo ajali ikitokea majeruhi wanastahili kulipwa.
Sasa, majeruhi wengi wanapoteza tiketi. Ambao ndio msingi wa madainya bima. Hata akiwa nayo inakuwa na jina tofauti na lake. Usumbufu mwingine ni kwa wenye basi kutokuwa na orodha kamili wa abiria waliokuwa kwenye basi wakati wa ajali. Manifest.

Kenya wanafanya. Ajali ikitokea, wanaojitokeza kwanza ni wanasheria kukusanya ushahidi wa kufanya madai ya bima. Hapa kwetu wanasheria wamelala wanaona usumbufu.
 
jana kuna basi moja mikoa ya kusini lilikuwa linakwenda mwendokasi wa kilomita 120 kwa saa
 
Back
Top Bottom