Wakati CCM wakiwa bungeni kupitisha bajeti, CHADEMA wako majimboni kwa mikakati

Wakati CCM wakiwa bungeni kupitisha bajeti, CHADEMA wako majimboni kwa mikakati

potokaz

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2011
Posts
540
Reaction score
493
Kwa hakika Chama hiki (CHADEMA)kina mipango, mikakati na dhamira ya dhati ya kuchukua dola. Wanajua njia waipitayo.

Msimamo wa mwenyekiti Mbowe ni thabiti na haujawahi kuyumba.

Wakati CCM wakiwa bungeni kupitisha bajeti, Chadema wako majimboni kwa mikakati madhubuti kidigitali kuipanda Imani ya chama kwa wananchi.

Yaani heri Chadema ya Bungeni kuliko hii iliyopo kitaa kwa sasa.

Inajijenga, inapaa, CCM hawakumuona holo. Fikiria kina Mdee wangekuwa nje ya Bunge nao. Huo mziki ungekuwaje?

Ila shetani akawadanganya dada zetu wale.

Ni dhahiri kuwa CCM sasa itawapasa wajiandae na wajipange na wasahau kabisa kutumia dola kubaki kwenye dola Kama walivyoelekezwa na katibu mkuu wao mstaafu, Dr.Bashiru.

Safari ya Tume Huru na katiba Mpya sio lele mama.

Washindani siasani wamekataa unyonge. Wameamua kupambana kwa hoja si vihoja. Wameamua kuiamsha ari ya nguvu ya umma unaowaunga mkono.
 
Ati CHADEMA kina mipango, mikakati na dhamira ya dhati ya kuchukua dola. Njia ni nyeupe kuelekea Ikulu 2025 iwapo tu Viongozi wa CHADEMA watachanga karata zao vizuri.

Badala ya kukipeleka Chama, ati kwa mikakati madhubuti kidigitali, watumie udhaifu wa uongozi wa sasa wa CCM. Kwa mfano wakati wa utawala wa Awamu ya Tano, Viongozi wa CHADEMA waliponda na kubeza mikakati yao ya kiuchumi kuwa ni "maendeleo ya vitu". Hayo maendeleo ndiyo yaliwagusa wapiga kura na kuirudisha CCM madarakani kwa kishindo. Huo ndio ukweli na viongozi wa CHADEMA wanaujua na hata Wabunge wa CCM wamepata kura kupitia huko.

Kwamba Uongozi wa CHADEMA una mkakati wa kuiamsha ari ya nguvu ya umma unaowaunga mkono! Huo mkakati usiwe kwa kupitia Safari ya Tume Huru na katiba Mpya ambao kimsingi nia na dhumuni kubwa ni UBINAFSI na UROHO WA MADARAKA wa Viongozi wa CHADEMA. Ni mkakati usio wa maslahi kwa wapiga kura. Huo ndio ukweli na Uongozi wa CHADEMA unajua.

Kinachopaswa kufanywa na Uongozi wa CHADEMA ni kuhakikisha Serikali ya Awamu ya Sita inaondolewa kwenye reli ya "maendeleo ya vitu". Kwa njia na jinsi ipi, naamini wanajua. Tayari zipo dalili, ndani ya CCM, za sintofahamu kuhusu mipango na mikakati ya "maendeleo ya vitu" hasa kumalizia "miradi ya mikakati" na kuboresha "huduma za jamii", kwa pesa za ndani.
 
Back
Top Bottom