Wakati dunia inafungwa, wewe fungua vitabu (vitabu 12 vya kusoma wakati unajikinga na virusi vya Corona)

Dah nifanyaje ili walau nisome kitabu, nikielewe, nikimalize ndani ya muda mfupi? Nitumie mbinu zipi wadau? Maana hali si shwari.
Tenga muda, kaa eneo tulivu na soma.
Andika yale muhimu unayojifunza kwenye usomaji huo.
Usiruhusu usumbufu uwepo wakati unasoma, hasa wa simu.
 
Sawa, kisome na usipanik kama wengi wanavyofanya sasa.
Napenda sana kusoma vitabu, lakini muda unanibana sana, ni vigumu kupata ratiba ya kunipa muda mrefu wa kusoma, Nikipata muda nalala kwa sababu ya kasi ya maisha na kuchoka, nilikuwa kijana mdogo nilisoma vitabu vingi sana na vimenisaidia mpaka leo. Natamani kuwa kama zamani lakini nashindwa.
 
Hakuna kinachoshindikana mkuu,
Kama uliweza kusoma ukiwa kijana, hata sasa ukiamua utaweza.
Nina hakika kuna mambo mengi unayafanya hayana tija, ukiyapunguza hayo utapata muda wa kusoma.
Lakini pia kuna mifumo mbalimbali ya kusoma, mfano kuna AUDIO BOOKS, hizi unaweza kusikiliza ukiwa unaenda au unarudi kazini, badala ya kupoteza muda ambao labda unakaa kwenye foleni au usafiri unakuwa unasikiliza vitabu.
Kama unahitaji hizo AUDIO BOOKS tuwasiliane.
Kila la kheri.
 
Aisee nazihitaji sana hizo Audio books, je vitabu ulivyorodhesha hapo juu vina audio zake?
Nazipataje?
 
 
Nafuatilia sana kazi zako mkuu, hongera kiukweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Tano; acha kufuatilia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Hali hii inakuzwa sana kuliko uhalisia wake, kama unataka kupata taarifa za maendeleo ya mlipuko huu tembelea sehemu zenye taarifa sahihi; shirika la afya na wizara ya afya.


Sehemu zinginezo niko pamoja nawe. Lakini kuhusu vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kwamba tusiifuatilie, mmmmm!
Sie wengine tunashinda humu JF kupata updates za covid 19, kwa hiyo tuache kuingia humu JF?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehemu zinginezo niko pamoja nawe. Lakini kuhusu vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kwamba tusiifuatilie, mmmmm!
Sie wengine tunashinda humu JF kupata updates za covid 19, kwa hiyo tuache kuingia humu JF?

Sent using Jamii Forums mobile app
Achana na habari zinazokufanya upaniki,
Wewe fanya kile kilicho sahihi kujikinga na maambukizi haya.
Kupaniki kutokana na habari hakutakusaidia lolote,
Ndiyo maana ni muhimu kuachana na habari.
 
ACHA KABISA KUTUMIA NA KUFUATILIA MITANDAO YA KIJAMII

Hapo nafikiri ingekua tutumie mitandao Kwa manufaa na uangalifu.

JF pia ni mtandao wa kijamii, ukisema acha kabisa kutumia na kufuatilia mitandao inamaana hata wewe haupaswi kuwa hapa, pia watu wasingevijua hivyo vitabu umependekeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…