Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Nasikia hii ilivunjika mwaka 1977. Nimekuwa nikisikia hadithi nyingi kuwa watu waligawana mali kama washenzi(barbarians). Hili limewapa baadhi ya watu vinyongo hadi leo kuwa walidhulumiwa, naomba kujua kwenye kugawana huko, Uganda alipata nini, Kenya alipata nini na Tanzania alipata nini?
Ufafanuzi uliyotolewa na Wadau
Ufafanuzi uliyotolewa na Wadau
(1)Azimio la Arusha halikuwa na athari kubwa katika uchumi wa Tanzania kabla ya EAC kuvunjika na nchi kuingia vitani. Mashirika mengi yaliyoundwa kumiliki mali zilizokuwa zimetaifishwa yalikuwa yakifanya vizuri sana; hiyo ni pamoja na STC, TCC, NDC, NMC, Mamlaka ya Mkonge, Mamlaka ya Tumbaku, mamlaka ya Pamba, etc. Athari za umiliki huo zilianza wakati wa vita baada ya uhaba wa bidhaa kutokea na kusababisha rushwa pamoja "bei za kuruka" kuanza. Ni wakati huo ambapo faida za kuwa na biashara binafsi zilianza kuonekana!
(2) Operation vijiji ilikuwa mwaka 1972-1973 hivi nikiwa primary school. Hii ilisababisha njaa kubwa sana mwaka 1974 na kuifanya serikali ipitishe sera ya Siasa ni Kilimo ili kuhamamasisha kilimo tena; njaa ile ndiyo iliyoleta mahindi ya yanga. Kufuatana na Siasa ni kilimo, mwaka 1976 nchi ilikuwa na chakula cha kutosha sana na khali ya kilimo cha mazo mbalimbali ilirudi katika msingi wake kabla ya mwaka 1973; kwa hiyo wakati EAC inavunjika mwaka 1977, Tanzania haikuwa na matatizo ya kilimo tena.
(3) Kuvunjika kwa EAC kuliathiri sana usafiri Tanzania kwa kiasi cha kutosha kuathiri uchumi. Usafiri wa ndege ulikufa kabisa kwa vile ndege zote zifungiwa Kenya kasoro ile iliyotorosha na kapteni mapunda. Usafiri wa meli kwenye ziwa Victoria ulikufa kabisa, ikabidi serikali inunue MV Butiama na MV Bukoba katika mazingira ambayo hayakuwa mipango ya serikali wakati huo, na usafiri wa reli pia uliathiriwa sana kwa vile karakana kuu ya reli ilikuwa Nairobi na mabehewa pamoja na vichwa vyote vilivyokuwa kwenye matengezo havikurudi, na mwisho hata usafiri wa barabara ulithirika sana kwa vile mabasi mengi ya masafa marefu wakati huo yalikuwa ya EAR yakisaidiwa na yale ya DMT