Wakati huu ni wa kujitihada kwenye vipaji. Ubunifu ulinisaidia katika wakati mgumu niliowahi kupitia

Wakati huu ni wa kujitihada kwenye vipaji. Ubunifu ulinisaidia katika wakati mgumu niliowahi kupitia

miamiatz

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Posts
505
Reaction score
941
Jitihada ni kulifanya jambo bila kuchoka wala kukata tamaa. Kipaji ni uwezo wa kubuni jambo ambalo lotawaacha wengine wabaki waoh.

Wakati huu ni wakati wa kuunganisha jitihada na vipaji ili kushinda ugumu wa maisha.

Kipaji huongeza kasi (speed). Jitihada huondoa uvivu. Kama unavyo vyote lazima utawin tu.

Kipaji na jitihada zilivyonisaidia wakati napitia magumu.

Ilikuwa nalazimika kwa siku kupitia websites 10 na makampuni na kuandika report ya findings and recommendations bila hata kuombwa kufanya hivyo.

Kwa mwezi nilikuwa napitia websites kana 250 hivi. Ilikuwa ni lazima nifanye haya masaa mengi sana.

Kila report niliituma kwa mtu sahihi wa kampuni husika. Mwezi wa kwanza nilipata kampuni tatu mabosi walinitafuta kwa simu na kuomba nifanyie kazi zile recomendatios. Nikaanza kupata pesa.

Mwezi uliofata nikapata kazi 7. Sasa ikawa kazi zinaanza kunizidia ikabidi nipunguze idadi ya report nnazotuma ili nipate muda wa kufanya kazi hizo ninazopewa.

Namshukuru Mungu nilivuka kipindi hicho kwa mtindo huo. Haikuwa kazi rahisi mana nilikuwa nikilala masaa sita tu kwa siku. Hii ndio inaitwa hard earned money.

Courtesy of miamiatz
 
Shukuru mungu ulikuwa wapata muda wa kulala...........mimi mpaka leo nalala chini ya masaa 6
 
mimi mbona nalala sana mzee...........matajiri wengi duniani wanalala kidogo kuliko hata mimi kapuku......tatizo ukiwa na mawazo ya mabillioni kichwani usingizi unakata wenyewe
Ni kweli mkuu, inataka kujitoa haswa!
 
Ni kweli mkuu, inataka kujitoa haswa!
natatizo linalotukabili wengi wetu ni kutoyaamini mawazo yako mwenyewe na kuwa ndiyo yaweza kuwa njia ama chachu yakuyaelekea mafanikio...wengi huwa tunakata tamaa bila ya kujua kuwa yaweza kuwa tumeliacha wazo lakipekee na bora zaidi katika maisha yetu na ulimwengu
 
Kabisa kabisa!
 
Back
Top Bottom