jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 36,197
- 29,717
Hii ndio tofauti ya Taifa huru na linalotambua maana ya kupata uhuru.
Leo hii Taifa letu linaletewa mjadala wenye akili kubwa na wenye mrengo wa kujikomboa kiuchumi bila kupangiwa na mkoloni.
Hongera sana kwa mhe.Rais kwa kutuletea mjadala wenye tija yaani ni namna gani nchi itapata fedha za kujitegemea na kujiondoa kwenye makucha ya wadhalimu na wakoloni mamboleo.
Mhe Rais anaunda tume ya kumshauri ni namna gani kila aitwaye mtanzania atachangia katika maendeleo na sio kubweteka na kusubiri fedha za walami ambao hutuoa na kulazimisha tuwaabudu na kufuata wayatakayo na hata kutaka kutufundisha namna ya kushighulikia uhalifu.
Hii ni nia njema sana na apongezwe kwa dhati
Ameshafanya hivi katika eneo la uchangiaji huduma za afya...ameleta bima ya afya kwa wote ambao ni muarubaini wa uendeshaji wa sekta ya afya japo unakwamishwa sana na mamluki waliozoea kupiga fedha za wadau.
Kwa idadi ya watanzania waliopo,kwa idadi na fursa za rasilimali zilizopo Tanzania inajitosheleza na kusaza iwapo tukipata viongozi wenye muelekeo huu.
Tulianza awamu ya kwanza ...tukapunguzwa kasi awamu ya pili n.k lakini kama alivyo fisi tukarudi kwa kasi awamu ya tano...wakaamua kutukwamisha ila tumerejea tena awamu ya sita kwa uangalifu na kwa kujifunza zaidi.
HAKUNA HAJA YA KATIBA MPYA HAPA...BALI UTEKELEZAJI WA MIPANGO ILIYOPO ...naweza kusema ndio muelekeo sahihi.
Kamwe vijana wetu msiingizwe kwenye siasa za kipuuzi yaani ili uwe bora eti uwe ni mpiga domo na kutukana serikali.
By the way watazameni wote wanaowashawishi ni vizee vinavyoelekea kumaliza muda wao duniani ama ni vizee vitarajiwa ambavyo havina ushahidi wa kuwafanyia mema vijana au jamii...tuwaepuke kwa sababu wapo tayari kuchukua fedha za kuneemesha familia zao kwa kuanzisha vurugu itakayowaumiza milele.
Tutoe ushauri kwa Tume na Mhe Rais in an honest way ili kujenga Taifa huru na sio Taifa la mihemuko ya ku copy n paste.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!