Wakati muafaka kwa serikali kuchukua hatua za haraka

Wakati muafaka kwa serikali kuchukua hatua za haraka

murumbasi

Member
Joined
Dec 3, 2014
Posts
75
Reaction score
25
Leo tarehe 9 Januari, 2015 katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku katika kituo cha ITV ni MASIKITIKO MAKUBWA kuona wakulima wa miwa kukosa kuuza miwa yao kwenye viwanda eti kwa sababu sukari imefurika kwenye mabohari huku wakitupia lawama Serikali kwa kutodhibiti uingizaji holela wa sukari kutoka nje ya nchi. Mhe. Rais utakumbuka tulikuchagua kwa kishindo na ukatuahidi makubwa lakini kinachoendelea hivi sasa kinatusononesha sana sisi wananchi. Ulitueleza tutakuwa na maisha bora iweje sisi wananchi tunalima miwa lakini tunakosa pa kuuza eti mabohari yamejaa. Hawa wanaoingiza sukari holela kutoka nje ya nchi wanajulikana kwa sababu tunafahamu kuwa Serikali ina mikono mirefu kwa nini Mhe. Rais suala hili Serikali isichue hatua ya kukomesha tatizo hili. Wafanyakazi wengi wa viwanda vya sukari wamepunguzwa kwa sababu ya sukari kukosa soko. Sisi tulio watoto wako tunasononeka sana kuona kitendo hiki kikiendelea na Serikali iko kimya.
Tusaidie Mhe. Rais tunajua kauli yako itasaidia.
 
Siwa sikii ng,o mimi mwenyewe niliamua kuwahama natumia ya ujerumani yahapa hovyoo! hayana kiwango labda kwa kuwasaidia nije niongee na mwenyeji wangu huyu shijimpingi amewahi kuniambia watu wangu wanashida ya kutumia sukari chafu inayovimbisha matumbo, vilevile nikaongea na mwenyeji wangu wa afghanistani nikamuagiza afanye kila liwezekanalo kuingiza na kuuza sukari iliyo nyeupe haya Mahindi niliyoyapatia fursa yameitumia visivyo sasa safari hii Yataisoma namba.
Wananchi wangu mnisamehe sina jinsi ndo hali ilivyo.
 
Back
Top Bottom