kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
Lugha ya Kiingereza ni lugha ya mawasiliano katika sehemu nyingi duniani kuliko lugha nyingine yoyote.
Chombo kinachotumika katika kufanikisha azma ya kukieneza Kiingereza, ni pamoja na Shirika la Uingereza linalojulikana kwa jina laBritish Council.
British Council linatumika kuimarisha utamaduni wa Kiingereza na limefungua ofisi zake katika sehemu mbalimbali duniani.
Lengo lake ni kufundisha lugha ya Kiingereza na utamaduni wake kwanjia ya vitabu, filamu na vielelezo kutoka Uingereza.
Mataifa makubwa ya Ulaya na Asia kama Ujerumani, Ufaransa, Uholanzi, China , Japani, yametenga kipindi maalumu shuleni na katika vyombo vya mawasiliano kufundisha Kiingereza.
Ni kwa sababu hiyo, sisi pia hatuna budi kufundisha somo hili, siyo tu shuleni lakini pia kwa jamii nzima ya Watanzania wale ambao wanatoa huduma katika jamii.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk Shukuru Kawambwa aliwahi kusema kuwa ufundishaji wa somo la Kiingereza kwa shule zamsingi utaboreshwa. Hii inatokana na kuwapo kwa msaada wa fedha kutoka Uingereza.
Napenda kuwapongeza walioshirikikatika kutoa uamuzi huu wa busara,kwani Watanzania wengi wakiwemo wasomi, wanashindwa kuwasiliana na wageni kutokana naudhaifu wa kukitumia Kiingereza. Udhaifu huu umechangiwa na mambo mengi ambayo ni pamoja namtazamo wa kisiasa uliokuwapo huko nyuma kuwa Kiingereza ni lugha ya wakoloni na hivyo ikapuuzwa.
Haya ni makosa tuliyorithi ambayo hatuna budi kuyapiga vita. Hata hivyo, kufundisha Kiingereza siyo kupuuza Kiswahili. Lugha zote mbili ziimarishwe kwa kiwango kinachotakiwa. Tulenge kuwaandaa Watanzania wawe weledi wa Kiswahili, Kiingereza na hata lugha nyingine .
Wasomi wetu wawe na ujuzi wa kujieleza kwa ukamilifu zaidi, kwani wenzetu wa Afrika Magharibiwanaozungumza Kifaransa na wale wa Kaskazini wanaozungumza Kiarabu nao wanajifunza Kiingereza.
Mradi wa kufundisha Kiingereza kwa shule za msingi unafuatia mradi mwingine wa kufundisha lugha hiyo katika shule za sekondariulioanzishwa mwaka 1992 na kukamilika mwaka 1996.
Yako masuala mbalimbali ninayotaka kuyapendekeza ili kuufanikisha mradi huu. Awali ya yote wateuliwe wataalamu wa lugha ambao wamebobea katika taaluma ya lugha ya Kiingereza.
Wataalamu hawa wawe wamebobea katika sarufi na pia mbinu za ufundishaji wa lugha, kwa maana ya uzoefu wa kufundisha lugha.
Wapatikane wakufunzi kutoka katika vyuo vya ualimu, Idara ya Ukaguzi wa shule na vilevile katika katika Taasisi ya Elimu Tanzania. Wachaguliwe wale wenye ujuzi wa mtalaa wa somo la Kiingereza.
Ifahamike kuwa tunao wataalamu wazawa wa lugha, na baadhi yao ni wale waliostaafu na baadhi wako kazini. Wana uzoefu mkubwa wa mazingira ya elimu nchini na watakuwa na nafasi nzuri ya kufahamu mazingira ya kufundisha lugha hii katika nchi yetu. Kwa hiyo haipo haja ya kuwatafuta wataalamu kutoka nje ya nchi.
Uko utaratibu kwa wale wanaotuletea misaada kuja kuiendesha miradi hii, hata kama wako wazawa wenye ujuzi wa taaluma na uzoefu wa kutosha.
Kwanza wafanyakazi wa nje wakiajiriwa watalipwa mishahara mikubwa na marupurupu mengine kama kupatiwa magari, nyumba na mengineyo.Malipo ya gharama zote yanatoka katika mfuko huo huo wa mradi.
Kwa hiyo utaona kuwa asilimia kubwa ya fedha za wafadhili zinarudi kwao kwa njia moja au nyingine. Kiasi kinachobaki hapa nchini ni kiduchu, na hakiwezi kuwana athari kubwa kwa jamii ya Watanzania.
CHANZO: MWANANCHI