Gwele
JF-Expert Member
- Jun 7, 2016
- 2,604
- 3,319
Mara nyengine soka haieleweki
Na tuzo za soka za mchezaji bora duniani zimedhihirisha hilo.
Ni vigumu kujua utaanzia wapi, lakini tutachanganua kile kilichofanyika katika tuzo hizo zilizotiliwa shaka
Ni nini kilichokua kikifanyika katika kura ya tuzo hizo? Je kuna mtu anayeelewa kilichofanyika?
Je kikosi cha wachezaji 11 kilichochaguliwa na Fifa ndio bora zaidi duniani?
Tuanzie na mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah. Alifunga magoli 32 katika ligi ya Uingereza msimu uliopita na alitajwa kuwa mchezaji wa tatu bora wa Fifa upande wa wanaume akiwa nyuma ya Modric na Cristiano Ronaldo.
Basi ni kwa nini hakuorodheshwa katika kikosi cha kwanza cha wachezaji bora 11 wa Fifa?
Halafu kuna kuorodheshwa kwa kipa wa Man United David de Gea licha ya kutoshinda taji la kipa bora lililopewa Thibaut Courtois.
Na ni vipi beki wa kulia wa Paris St-Germain anayeuguza jeraha Dani Alves aliorodheshwa miongoni mwa wachezaji 11 bora duniani wa fifa?
'Huenda Sanchez akaondoka Man Utd'
Raia huyo wa Brazil alikuwa ameorodheshwa katika timu nane kati ya tisa akikosa kuorodheshwa mwaka 2014 pekee.
Je hakuna mabeki wengine wa kulia katika timu nyengine? jamani kuna yeyote?
Ni kweli kwamba kuna shaka miongoni mwa mashabiki wa kandanda kuhusiana na kuorodheshwa kwa baadhi ya wachezaji katika kikosi hicho cha Fifa cha wachezaji 11 wa kwanza, lakini kile ambacho tuzo hizo hazitegemei ni kuwa na msimamo.
Fifa imeelezea vile kura hiyo ya kumchagua kocha bora na mchezaji bora zilivyofanyika - manahodha wa timu za taifa , wakufunzi wa timu za taifa , baadhi ya waandishi na kwa mara ya kwanza kura ya mashabiki iliopigwa katika mtandao huku kila moja ikiwa na asilimia 25.
Lakini Fifa haijaelezea ni kwa nini Salah na Courtois wanaweza kuorodheshwa katika kikosi cha pili cha wachezaji 11 bora wa Fifa mwaka huu.