Wakati mwingine watu hawasemi pole

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Wakati mwingine watu hawaamini kuwa walikosea. Lakini hiyo haijalishi. Kuomba msamaha sio kukuthibitisha kwamba umekosea la hasha bali unajitetea mwenyewe.

Usisubiri mtu akuombe msamaha na kumwekea kinyongo hadi atakapofanya hivyo.
Unajua kwa nini? Kwa sababu mtu ambaye anahisi hasira yako, hufadhaika, na kujenga chuki na wewe ama kukuogopa na kukukwepa.
Hisia hizo za uhasama, mihemko, na mawazo hutiririka kupitia mkondo wa damu yako kama sumu yenye nguvu kubwa na unakuwa mwenyeji hai wa sumu hiyo.
Badala ya kungoja msamaha, au kutarajia mmoja aje, tambua kuwa huenda isitokee na ni sawa. Kwa sababu maisha yako na furaha yako haitegemei mtu mwingine kusema samahani. Maisha yako na furaha yako inategemea wewe na si mtu mwingine.
Kwahiyo hata kama wakati mwingine wasipokuomba msamaha wala kukupa pole usijali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja
 
Tenda wema na ukwende zako usingoje shukrani..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…