Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Allien utakuwa unamuangalia JK kwa jicho moja....Inapaswa uwe makini sana na huyu Muungwana,Yeye anajua kila kitu kinachoendelea kwenye sakata hilo la Masha Vs Mengi.Kama kawaida yake kwenye mambo mengi anajifanya hausiki...Hakuna anayeweza kutoa kauli "siku saba" zimekwisha na Bwana Waziri yupo Switzerland (Geneva),Kuna habari kuwa anarudi Tanzania Kesho....Ngoja tusubiri!!!
Muungwana kama ilivyo Mugabe Nchi imemshinda......
Kiongozi Mwawado;
Najizuia sana kutaka kujua nini hasa kiliongelewa katika katika hivyo vikao vya siri vya kumhujumu Mengi (Any way kama kweli vilikuwepo):
Je JK alikuwepo na je anajua kinachoendelea?
Kama anajua, je hii Tuzo aliyopewa Mengi na JK (sijui ni ipi) labda kwa ajili ya mchango wake kwa taifa, je alimezea tu wakati wa kumpa lakini moyoni anajua lazima tumfilisi Mengi?
Kama hajui, je inawezekana kijana wake Waziri Msomi amechezea rafu Mengi na yeye JK amekuja tu kusikia tu katika Media?
NB: Check distance ya kupeana mikono kati ya Muungwana na Bwana IPP!!
Rais JK siku ya Jumanne alimtunukia Bw. Reginald Mengi pamoja na watu wengine Nishani mbalimbali kama inavyojieleza katika picha.
Source: Guardian of 11th December 2008
habari hii si ya kweli. mimi nilihudhuria sherehe hiyo ikulu. waliotunukiwa nishani walikuwa askari wa JWTZ, POLISI & MAGEREZA. Raia pekee alikuwa mh. Benard Membe pekee kwa vile alikuwa kiongozi wa mawaziri wa nje wa AU ambao niyo walipendekeza kupeleka wanajeshi comoro na yeye akawa na jukumu la kusimamia mpango huo. otherwise, kina mama wawili walienda kuwapokelea waume zao (maaskari) nishani kwa vile waume ho ni marehemu kwa sasa .
R. Mengi alikuwa mwalikwa tu kama wengine na si kupokea nishani. jamani tuweke heshima ya JF kwa kuandika ukweli hapa
Lakini kwa upande mwingine, nashindwa kuelewa kiwango halisi cha influence aliyonayo huyu 'waziri kijana' kwa mh.Rais. Inawezekana nikawa nimeteleza lakini inasemekana watoto wawili wa marais wetu, mmoja wa kule visiwani na mwingine wa Muungano ni waajiriwa wa kampuni ya kisheria ambayo bw.Masha ana hisa kubwa. Conflict of interests? sijui!!
Lakini kwa mfumo ulivyo nchini kwetu, sio rahisi ati rais hana taarifa kabisa na mikakati hiyo. Na kama atakuwa anafahamu mikakati hiyo na asichukue hatua zozote, basi itatuletea maswali kuhusu udhati wa vita yake dhidi ya mafisadi.
Kiongozi Boma;
Kwanza Usini-question juu ya heshima kwa JF juu ya kuandika ukweli. Sijaandika Uongo na ndio maana unaona title ina question mark.
Pili nimekuonyesha source ya habari na kuna picha ambayo inajitosheleza kwa maelezo, hivyo badala ya kuniqu-estion juu ya ukweli, question juu ya source na mwandishi wake na elezea juu ya credibility ya huyo mwandishi badala ya kunituhumu kutokuandika ukweli. I hope moderators watali-observe hili.
Binafsi jana niliona sehemu fulani katika kipindi cha TBC cha Jambo Africa lakini niliona sehemu tu sherehe hizo hasa pale askari walipokuwa wanatunukiwa.
Hata hivyo bado kuna maswali ya kimsingi juu ya ufahamu na Uhusika wa wa Muungwana katika sakata la Waziri Kijana na Mzee IPP.
nasdhani hakuja hana ya malumbano kwa hili. Ukweli ni kuwa mengi hakutunukiwa nishani yoyote, hivyo question mark kwenye mada inaweza kuondoka kwa kuwa jibu limepatikana. Na baada ya kujulikana kwa ukweli huo, je, mada hii bado inaswihi kwa jinis ambavy0 ilivyo?
Mkuu Allien utakuwa unamuangalia JK kwa jicho moja....Inapaswa uwe makini sana na huyu Muungwana,Yeye anajua kila kitu kinachoendelea kwenye sakata hilo la Masha Vs Mengi.Kama kawaida yake kwenye mambo mengi anajifanya hausiki...Hakuna anayeweza kutoa kauli "siku saba" zimekwisha na Bwana Waziri yupo Switzerland (Geneva),Kuna habari kuwa anarudi Tanzania Kesho....Ngoja tusubiri!!!
Muungwana kama ilivyo Mugabe Nchi imemshinda......
Mengi asubiri misuli ya Masha
Na Ramadhan Semtawa
Lakini inaonekana Mengi ametunisha msuli kusubiri kuona waziri huyo akichukua hatua hizo.
Hadi jioni saa 11:30 jana, Mengi hakuwa amewasilisha uthibitisho huo, si wizarani wala makao.....