Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Kila siku nasema.
Tatizo letu Tanzania sio uwepo wa rasilimali bali ni kuwa na watu wenye akili sahihi za kutupeleka kuwa nchi ya ahadi.
Wakati Tanzania yenye utajiri wa gesi kiasi cha ujazo wa trilioni 57 ikiendelea kuagiza mafuta kutoka nje tena kwa fedha za kigeni ili kutumia kwenye magari yake na viwanda, Nigeria wameona watumie akili zao vizuri kwa kuagiza magari nchini humo kubadilishwa mfumo kutoka petrol kwenda kwenye gesi ambayo inapatikana kwa wingi kwao ili kuondoa utegemezi wa kuagiza mafuta kutoka nje na kuokoa fedha za kigeni.
Naionea huruma sana Tanzania yangu. Sijui lini tutapata Viongozi wenye akili watutoe hapa tulipo.
Yaani pamoja na kugundua gesi yote hiyo hadi leo kwa Dar tu tuna vituo vya kujaza gesi magari vizivyozidi 4. Alafu Viongozi wetu hawa kila siku wanatembeza bakuli kuomba fedha za miradi ya maendeleo nchini kwetu wakati tungeweza kuokoa fedha nyingi sana tunazotumia kuagiza mafuta kwa kutumia gesi yetu hii kwenye magari na viwanda.
Kweli bongo nyoso.