Wakati tukiwa bize kupiga vita masuala ya ushoga nchini mwetu, hili nalo tulitizame

Wakati tukiwa bize kupiga vita masuala ya ushoga nchini mwetu, hili nalo tulitizame

crankshaft

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,427
Reaction score
3,438
Watoto wa kiume katika media na mitandao hapa Bongo kusifia au kukandia kazi za wanaume wenzao.

Haiji akilini kabisa mwanaume kabisa na madevu yake, mume wa mtu, yeye kila siku yupo bize kumsema na kukusoa juhudi za mwanaume mwenzake. Wana maana gani hawa kwenye jamii zetu? Si suala lilelile tu? Yanajiita machawa sijui

Nijuavyo moja kati ya sababu watu hawataki haya mambo ya ushoga ni ku-consolidate tabia za kiume miongoni mwa vijana wa kiume katika jamii zetu, sasa ni tabia gani wanatuonesha baadhi ya hawa wanaume katika media na mitandao hapa nchini?

Hivi wanajisikiaje wake zao hawa watu? Wanajiona wana waume kweli? Yaani mumeo anapata ugali wake kwa kuchamba wanaume wenzie ambao hawajamkosea chochote? Hapana aisee inatia aibu hii.halafu ni Bongo tu haya mambo.

Jamii kila siku inapiga kelele masuala ya ushoga lakini imekumbatia watu kama hawa maana yake nini?

Hili nalo tulitazame aisee.
 
Sasa watu na akili zetu tukae JF kuwajadili wapumbavu aina ya Mwijaku?

Hebu tuache kwanza.
 
Wewe unabidi Kujitambua usiwape wapumbavu nafasi ya kuwafatilia.
 
Si vibaya watu Kama wa hivyo wasipo semwa hawawezi kujifunza au kuacha, Ile mibaba yaovyo kweli, kuchamba juu ya juhudi za wenzao.
 
Back
Top Bottom