Wakati tunamshukuru alivujisha mkataba, tujiandae pale watakapozima mtandao!

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Kuna hisia nazipata hasa baada ya DP World kufunga message huko instagram. Watanzania wamekuwa wakionesha hisia zao kuhusu kutokubaliana na mkataba wa kubinafsisha bandari kwa muda usio na kikomo. Wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kudhihirisha hisia hizo.

Sasa hofu yangu kwa sasa ni juu ya suala zima la kuzimwa kwa mtandao (internet) Sijui itakuwaje? Tunasaidiane ndugu!

Nakumbuka 2020 tulitumia vpn pale walipozima mtandao; japo wengi walikosa mawasaliano.
Watanganyika kwa sasa tunapitia changamoto ya kutaka kulinda rasilimali zetu ambazo tumepata kwa kudra za Mungu.

Je, tuendelee kunyamaza tusihoji?
Je, tuishi tu kama tusiojua jema na baya? Nini kifanyike?

NB: nimetafakari hili baada ya kumsikia mwanaharakati mmoja akilalamika kupata taabu kuendesha space huko twiter. Aidha huku nilipo pia mtandao upo chini na wakati mwingine unapotea kabisa jambo ambalo si la kawaida sana!

Pia soma>> Watanzania wamefungiwa internet
 
VPN,, Please,,!

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Ni vile tu Kila kitu tutumiacho si chetu Kwa 92%, utandawazi...... ukoloni mamboleo..... wakubwa ni wakubwa tu wajamen......kula nyama nyamaza🙆
 
Yaani wazime mtandao kisa huu mkataba..??? Sahau kuhusu hilo kutokea, hili limeshaisha, mengine yanafuata tujenge nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…