
Ndugu Zangu,
Wakati Watanzania kwa maelfu wamefunga safari kwenda kwa ' Babu' Loliondo, kimwili, kiakili na kiroho,kuna wengine wajanja wana safari yao.
Ndio, sasa Watanzania kwa mamilioni wamehamia Loliondo. Kama hawako njiani kwenda huko, basi, wanaongelea Loliondo. Hivyo basi, wameshafika kwa ' Babu', Talk about philosophy of mind!
Na kuna mambo ya msingi kabisa tumeshayaweka kando. Angalia hayo ya pichani. Jarida la The East African limekuja na habari kubwa. Kesho litakuwa mitaani. Mie nimebahatika kulikamata leo. Lakini ah! Ni Watanzania wangapi watakaolisoma jarida hili katika wakti huu wa kuhangaikia nauli za kwenda kwa ' Babu' Loliondo?
Labda ndio maana, Baba Askofu Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo ameongea kwa uchungu jana; kuhusu Dowans, amehoji kwanini Serikali ilazimishwe kuilipa Dowans.
Na Baba Askofu akasema; " Kuna baadhi ya viongozi ndani ya Serikali wamekuwa wakitenda mambo mengi mabaya dhidi ya wananchi na kuyaficha kwa gharama yoyote".
Hayo ni maneno mazito kutoka kwenye kinywa cha Baba Askofu. Swali linabaki, ni Watanzania wangapi wamemsikia Baba Askofu Kadinali Pengo?
Maggid
Dar es Salaam
Jumapili, Machi 13, 2011
mjengwa