MKAKA WA CHUO
Member
- Aug 13, 2022
- 11
- 6
Katika maisha yetu ya Kila siku Kila mtu anatamani awe na mafanikio katika Nyanja moja ama nyingine.kiuhalisia mafanikio ni ndoto ya Kila binadamu mwenye akili timamu. Mafanikio hayo yanaweza kuwa ya kielimu, kiuchumi, kisiasa, kiimani, kiafya na kimichezo. Ni jambo lisilopingika kwamba mafanikio hayo ambayo hutafutwa na kupambaniwa na jamii zetu Huwa na Lengo kubwa moja , nalo ni Kuishi kwa Raha na Amani.
Katika upambanaji na utafutaji wa mafanikio siyo watu wote wanaopambana hufanikiwa, jambo hili linaweza kutokana na namna ya upambanaji, mazingira ya utafutaji, Hali ya vifaa vinavyotumiwa katika utafutaji na kadhalika, jambo hili ni lakulizingatia katika maisha kwasababu haitakuwa sawa kusema maskini wote siyo wapambanaji, lakini jambo la kuzingatia ni kujua kivipi watu wanatakiwa kupambana na kuendesha harakati zao kulingana na MDUNDO.
Mafanikio ni Lengo ambalo linahitaji uchaguzi sahihi wa njia ambayo mtafutaji ataitumia ili kulifikia Lengo Hilo la mafanikio.Kwa kawaida uchaguzi wa njia hiyo utategemeana na vitu au SABABU tofautitofauti Kama vile Afya, uchumi, elimu, malengo ya baadae na jinsia, hivyo basi Kila mmoja wetu katika jamii anatakiwa achague njia ya kupita kuelekea kwenye KITUO Cha mafanikio kulingana na Hali yake binafsi ya kiafya, kiuchumi, na kadhalika na hiyo ndio midundo ya kuzingatia kabla ya kuamua kuanza safari ya kutafuta mafanikio.
MDUNDO katika mziki ni ala ambayo inamuongoza mchezaji namna ya kucheza, ikiwa MDUNDO unaenda taratibu na wewe mchezaji itabidi ucheze taratibu, vilevile MDUNDO ukiwa unaenda kwa haraka na mchezaji itabidi ucheze kwa haraka.
Hali na malengo ya Kila mmoja wetu katika jamii ndio inatakiwa imuongoze katika kuchagua shughuli ya kufanya ili apate MAENDELEO. Kwa mfano kijana mwenye malengo ya kuwa daktari ni lazima asome masomo ya sayansi kinyume na kusoma masomo ya sayansi hatokuwa na vigezo vya kusomea udaktari, kiuhalisia Kila kitu kina hatua zake za msingi za kufikiwa Kama ilivyo ili uwe daktari lazima usome masomo ya sayansi.
Vilevile wakulima,ili uweze kuenda vizuri katika kilimo chako lazima ulime eneo ambalo unauwezo wa kulihudumia, kwa mfano mkulima ana shilingi milioni mbili alafu anahitaji kupanda nyanya hekari sita, nyanya hizo zikishaota zitahitaji kumwagiliwa maji kwa muda wa miezi mitatu kabla ya kuanza kuvuna, zitahitaji kupaliliwa mara mbili au zaidi, zitahitaji dawa za wadudu Kila baada ya wiki mbili, mbolea ya kupandia, mbolea ya kukuzia na mbolea ya maua na matunda zote zitahitajika, kutokana na kutokucheza kulingana na MDUNDO mkulima huyu atashindwa kulihudumia eneo hili kwasababu ni kubwa kuliko kiasi alichonacho hatimaye atapata hasara katika shughuli yake hii.
Wakati mwingine katika jamii zetu unaweza kukuta familia zenye uwezo duni wakiuchumi wanalazimisha kupeleka watoto wao katika shule binafsi kwa Lengo la kujihakikishia ufaulu wa watoto wao, hili ni Lengo zuri lakini kutokana na kutokucheza kulingana na MDUNDO wa mziki wako, mwisho wa siku unaweza ukajikuta unapata hasara na maumivu makubwa kinyume na ilivyotarajiwa, kwa sababu kitendo cha kumpeleka mtoto shule binafsi lazima ujihakikishie uwezekano wa kupata ada na mahitaji mengine lakini Kama itakuwa mtoto amepelekwa shule binafsi kwa SABABU ya MTU Fulani ambaye amempeleka mwanae kwenye shule binafsi, jambo hili litakuja kutuletea madhara makubwa mbeleni iwapo kutatokea Hali ngumu ya upatikanaji wa Ada, na mahitaji mengine ya msingi Kama pesa za michango,sabuni na kadhalika kwasababu kukosekana kwa Ada kutasababisha mtoto kurudishwa nyumbani, kukosekana kwa michango ya shule na vitu vingine Kama sabuni na pesa ya mkononi kwa mwanafunzi kunampa mazingira magumu ya kusoma, hatimaye wazazi wanaweza kuwa wanapambana Sana kulipa Ada na michango lakini kutokana na mazingira ya mtoto hapo shuleni bado hayamfanyi aweze kufaulu kwasababu unawezakukuta mwanafunzi Hana mafuta ya kupaka, sabuni,mswaki umeisha, daftari la hesabu limeisha na mwalimu wa hesabu ni mkali na kadhalika, kutokana na mazingira Kama hayo kwa muda mwingi mtoto huyu anakuwa katika hali ya mawazo na siyo kusoma, hivyo wazazi kabla ya kuchagua shule za kupeleka watoto wenu lazima mzingatie uchumi wenu na Hali za kifamilia.
Vilevile kwa wanafunzi wa ngazi zote kwa ujumla, kwa kawaida Kila mwanafunzi anapenda na anahitaji kufaulu vizuri, lakini Sasa wengi katika sisi wanafunzi hatufati njia za kufaulu, kwa mfano wanafunzi wengi wa vyuo vikuu tunatabia za utoro hivyo mkufunzi anapofundisha Kama wewe haupo hauwezi kufaulu jaribio, Kuna wengine wanaweza kuwepo lakini hamsikilizi mkufunzi Bali yeye anacheza gemu kwenye simu yake na foni zake kachomeka masikioni na kadhalika, hivyo kutokufata hatua stahiki za kufaulu huko ni kwenda kinyume na MDUNDO na ndio maana inakuwa vigumu kwa wanafunzi wengi wa vyuo vikuu kupata ufaulu mkubwa.
Wanamichezo, wengi katika wanamichezo wanapenda kuwa na umaarufu na mafanikio makubwa katika michezo, jambo linalosikitisha baadhi katika hao wanamichezo hawataki kufanya mazoezi yaani wavivu, Sasa huku ndio kucheza kinyume na MDUNDO, kwasababu hakuna mchezaji mkubwa ambaye ni mvivu kwenye mazoezi, lazima wachezaji wetu wajue kwamba unaweza kuwa na kipaji Cha Mpira wa miguu, kikapu na kadhalika lakini Kama haufanyi mazoezi utapitwa na MTU ambaye Hana kipaji Cha Mpira wa miguu,kikapu na kadhalika kwasababu yeye anafanya mazoezi mengi kukuzidi wewe mwenye kipaji, Kumbuka kipaji kitazidiwa na jitihada Kama kipaji kitabakia bila jitihada, ukiwa Kama mchezaji hakikisha kocha anakosa mbadala wako.
Lakini vilevile namna ya Kuishi, Kila mmoja katika jamii anatakiwa Aishi kutokana na Hali yake ya kiafya na kadhalika, kwamfano mama mjamzito anaposhauriwa na daktari kuwa anatakiwa afanye mazoezi basi lazima afanye hivyo na huko ndio kutakuwa kucheza kulingana na MDUNDO, kinyume na hivyo atakuwa anajiweka katika mazingira hatarishi yeye mwenyewe binafsi, vilevile watu wenye ugonjwa wa kisukari inabidi waepuka vyakula wanavyoelekezwa , na watu wenye uzito mkubwa na MATATIZO mengine inabidi waishi kulingana na maelekezo ya madaktari ili kuhakikisha usalama wa Afya zao binafsi, kinyume na kufata maelekezo hayo, itakuwa sawa na kupishana na MDUNDO na mwisho wake madhara yatawarudia wenyewe.
Picha za hapo chini ni vichwa vya habari kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo jamii forum. Baadhi ya WATANZANIA wana agiza mizigo mingi nje ya nchi alafu wanashindwa kuilipia ushuru inabaki bandarini, na huko ndio kucheza kinyume na MDUNDO. NDUGU ZANGU WATANZANIA,TUTIMIZE MAJUKUMU YETU,TUFANYE MAMBO TUNAYO TAKIWA KUYAFANYA NA TUISHI KUTOKANA NA HALI ZETU, ZINDUKA.!! USILAZIMISHE KUFANANA NA WATU, KUMBUKA TUMEUMBWA TOFAUTI NA HALI ZETU PIA NI TOFAUTI.
BY: MKAKA WA CHUO.

Upvote
0