Wakati wasanii wetu wanafanya show na wanasiasa, Davido apiga shows na 50 Cent na Chris Brown

Hijajibu swali Narudia tena Diamond aliombwa kupaform kwenye lile tamasha na waziri wa habari Mh Mwakiembe ili aliwakilishe Taifa je,ulitaka akatae?

Aliperform wapi na katika shughuli gani na ni wapi nimesema Diamond akatae kuperform akiambiwa na Mwakyembe?

Usidhani kila mtu anafuatilia kila anachokifanya Diamond, sijui unaongelea nini.

Pokea ushauri au tembea. Una uhuru wa kubaki gizani.
 
Uzi wa kidwanzi.Acha kuwatukuza wamarekani.

Maneno haya yanasemwa na mtu anayejiita Pacbig huku avatar yake ikiwa picha ya 2Pac. Niambie sasa nani anawatukuza wamarekani.

Wewe hauna tofauti na huyo jamaa wa juu. Sijui hata kama nilichoandika umekisoma. Ungesome usingetoa comment kama hiyo.
 
Ahaaaaaaah mimi nilizania wewe ndiye baba yake davido maana umempamba sana balaaa

InshAllah na mimi nitakuwa bilionea hivi karibuni.

Davido yuko juu kimuziki hahitaji kiki ili awe kwenye headlines. Ila tusiende huko tafadhali.

Mada ya leo ni ya kutoa ushauri ili muziki wetu ukue na wasanii wetu watoke kwenye makucha ya wanasiasa. Ila inaonyesha wabongo bila drama maongezi hayanogi.
 
Haka ka uzi kana point na ukwel ndani yake ila ngoja tukapinge vikali tena bila point ,, buana davido yule jamaa ana pesa huwez kufananisha na mond
 
Heee! We jamaa vipi?! Kama hujui namna mijadala ya kwenye forums inavyoendeshwa ngoja nikujuze! Mtu anaweza ku-comment kutokana na mada kuu au anaweza ku-comment kutokana na posts zinazochangia mada kuu!!

Nime-comment kutokana na post yako. Na hata baada ya ku-comment, ulijaribu kuijibu... kwanini basi uliendelea kujibu kama ulitaka watu wajadili mada kuu?!

Utakuwa mtu wa hovyo na wa ajabu ikiwa ulitarajia watu wasi-comment kutokana na posts zako! Btw, ina maana hilo unaliona sasa?! Au kwavile umeshindwa ku-defend hoja yako?!

Btw, ubishi ni kukuambia there's no way huyo Davido or any Nigerian Musician anaweza kushiriki kwenye Power series ambayo ipo ukingoni?! I repeat... NO WAY!!!

All in all, who are you upangie watu cha ku-comment?!
 
Kwa hiyo mtu akipiga collabo na Fifty Cent kwako ndio mafanikio?

Kisa Fifty ni Mmarekani.Watu kama nyie ndio mnawafanya Wamarekani wajione First Class citizen.

Msanii akipiga Show kuwaburudisha Watz wenzake unamdharau, ila akiwaburudisha Wamarekani unamuona wa maana.

Una akili za kitumwa.

Kuhusu kuweka picha ya 2pac kama avatar haiwezi kuwa sababu ya kwamba nawatukuza.Ungeuliza kwa nini nimeiweka upate sababu?
 

Hahahahahahahaha!!!! Dahhhhh!!!!!

We jamaa una kipaji cha kuchekesha. Sasa mada kama hii tu ya kuelimishana unatoka jasho na povu hivi je ningekuja na mada za kumteketeza na kumbomoa mtu wako hapa si ndiyo ingekuwa balaa?

Ila this is too funny!!!

NB. Wenzio wamechukua ujumbe unaowafaa wanaenda kuufanyia kazi wewe umekaa hapo unabwabwaja mambo yasiyo na kichwa wala mguu. Ila wengine mambo mengine haya tunayafanya bila kitegemea shukrani za wanadamu, bila hivyo.....
 

Alikuwa mkubwa, not anymore. Siku hizi kabaki kusutana instagram tu
 
Alikuwa mkubwa, not anymore. Siku hizi kabaki kusutana instagram tu

Nature ya industry na ya ucelebrity imebadilika ila kiufupi 50 Cent bado ni msanii mkubwa kwa kila vigezo unavyoweza kuvitumia.

Ila kama nilivyokiri toka mwanzo, binafsi siyo mfuatiliaji sana wa muziki wake kwa sasa ila ukiwa mazingira ya aina fulani, muziki wake ni PERFECT kuutwanga.
 
Umetema madini gani zaidi ya akili za kishamba kuamini mafanikio ni mpaka upate American appreciation.
 
Wakati hao wasaniii wa bongo wakipiga mingo kwa kuwatumia wanasiasa, kun mtu humu jf hana lakufanya bali kutoka povu.
 
Usilazimishe, fiftty aliisha toka 2010.
 

Nilikujibu kukupa heshima kama mchangiaji ila nikakujulisha tubaki kwenye hoja ya msingi. Sijashindwa kudefend jambo lolote, usilazimishe.

Wawili au watatu mnaong'ang'ania upuuzi mnaoandika mnasound kama huyo jamaa anayelike comment zenu joseph1989. Multiple IDs?
 
Wakati hao wasaniii wa bongo wakipiga mingo kwa kuwatumia wanasiasa, kun mtu humu jf hana lakufanya bali kutoka povu.

Nimekumbuka hekima za wahenga zinazosema 'usimuamshe aliyelala, utalala wewe'.

Katika hili ngoja nizitumie hekima hizi.
 
Niwe na multiple ID ili iweje? Au namuogopa nani?

Tatizo lako hupendi kupingwa ,kujibu hoja za wenzio,umeulizwa maswali hujajibu,ila unapenda watu wajibu hoja zako.

Kuna thread yako moja nilichangia nilikuuliza maswali zaidi ya kumi hukunijibu zaidi ya kurukaruka na ndio maana hata ulivyonitag asubuhi sikutaka kuchangia sababu najua una akili ndogo.

Hizo comment zote nilizo like jamaa wapo sawa,tatizo hujui alafu ubaya zaidi HUJIJUI KWAMBA HUJUI.Usiku mwema ,ila sitochoka kulike 😎😎😎😎😎😎😎😎😎😎.
 
Umetema madini gani zaidi ya akili za kishamba kuamini mafanikio ni mpaka upate American appreciation.

Baada ya maelezo yooote niliyotoa, umeng'ang'ania mambo yasiyo ya msingi na somo lenyewe halijakuingia unaendelea kushikilia ujinga wako.

Ungekuwa darasani, bakora zingekuwa zinakuhusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…