Wakati Watanzania tunakimbizana kuchagua viongozi wanafiki Kenya wanachagua waleta maendeleo

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Wana FJ,

Kwa kweli ukisikia kuachwa ndio huku, wakati sisi tunaangaika huku na huku kuchagua viongozi bila kuzingatia vigezo na masharti hadi kufikia kuchagua viongozi walio na mazoea kula rushwa na kujilimbikizia mali, Kenya wako bize na mikakati ya kuendeleza nci yao kiviwanda, kibiashara na kiuchumi kwa ujumla.

Kusema ukweli pamoja na kwamba uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi ya kwenye vitabu na danganya toto ya wageni wanaotaka kuingia nchini kujichukulia walichokibakiza wakati wa ukoloni. Sifa nyingi tunapewa lakini wakenya wanafanya kwa vitendo.

Hapa nchini ni baadhi ya barabara zao, barabara ndio njia kuu ya utandawazi wa kuendeleza uchumi.
 
Hakika,kwa viongozi hawa wa mazoea na mfumo wetu wa kiutawala na kiutendaji,tunahitaji miujiza ili kuwafikia wa-Kenya
 
Wa TZ kazi yetu kubwa kutangaza nia baada ya kugundua Ikulu kumbe unaweza tu ukafanya biashara kama kawaida tena kwa ulaini zaidi
 
We vipi? nyie si mnapita majukwaani mnawadanganya wananchi kwamba barabara zilizojengwa na ccm sio kigezo cha maendeleo!? leo unakuja na propaganda zile zile! kwani Tanzania imejenga barabara mpya ngapi!? pita mikoa ya kusini uone, watu walikua wanasafiri wiki, na sasa hivi Magufuli ameshasaini utengenezaji wa flyovers lakini wapinzani wanapinga bajeti yake, sasa unataka nini!? Daraja la kigamboni pia hujaliona? watu wengine bana!
 














[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD="class: alt2"]





[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

If it forms a complete loop, then it is a roundabout even though it might not be referred to as such.
 
Barabara zipi za viwango vipi, hiyo ni sawa na kupaka rangi kokoto na kushindilia unasema ni lami, mvua moja tu kokoto zote bondeni katikati kunabaki mashimo, vyanzo vya ajari tayari.
 













[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD="class: alt2"]




[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

If it forms a complete loop, then it is a roundabout even though it might not be referred to as such.
Umenitoa michozi, lakini kwa kuwa mitanzania ndivyo tulivyo basi ngoja tufe kwa kusononeka tu.
 
Barabara zipi za viwango vipi, hiyo ni sawa na kupaka rangi kokoto na kushindilia unasema ni lami, mvua moja tu kokoto zote bondeni katikati kunabaki mashimo, vyanzo vya ajari tayari.

Una ugonjwa wa Tanzaphobia.
 
Ni kwamba Kenya ina wasomi wengi kuliko Tanzania. Tanzania ina majungu mengi kuliko Kenya.
 
Tz hakuna tofauti ya professor na std 7..woote akil sawa 2.kila mtu anaweza maendelea ni kuwa na nyuma pamoja na gari basi...et wanaita (kutoka)...
 
Kenya wamatuzidi mbali, tumuombee prof. Muhongo apewe ridhaa tuanze kuifukuzia kenya
 
Kama kigezo cha kugombea urais Tanzania ni kama nilichokiona kwa mmoja wa watia nia eti amewahi kutoa maoni ya kuomba Bunge Maalumu la Katiba lisitishwe basi Watanzania hatuna namna ingine bali kubaki wasindikizaji tu katika suala la maendeleo.
 
construction of SGR ahead of schedule! Tanzania maneno maneno tu.
 
Ukiangalia historia yetu ya Kenya tumekuwa na rais wa nne na vyama vitatu vimechukua uwongozi, maraisi wetu wawili wa kwanza hawakusaidia wananchi sana, walikuwa wanawakilisha familia zao, maendeleo kidogo tulioyapata hivi majuzi yamekuja na mzee Mwai kibaki, yeye ndie aliye jenga msingi /blue prints ya development wanayoitumia viongozi waliopo madarakani hivi sasa. katiba pia imechangia pakubwa kwa utenda kazi. Kenya na Tanzania hatujawachana mbali, kura yako ni haki yako na sisi kama waafrika tukijua nguvu ya kura, tutapata maendeleo. si shabikii chama chochote lakini kusema ukweli, ni wakati wakujaribu chama nyingine, kama hawata perform, then tutatumia hio hio kura kumtafuta mzalendo anayeipenda nchi yake. Kenya bado tuko na njia ndefu ya kuenda, lakini tunajua tuna uwezo na wale viongozi waliopo madarakani wanajua tunaweza kuwabadilisha ikibidi. watu wengi humu husema waKenya tuna misifa, sikatai, lakini ukiangalia tulipokuwa miaka kumi na mbili iliopita na pahali tulipo sasa, hatuna budi ila kufurahi, tunajua tunaweza na tumeona matunda ya raisi anayetaka maendeleo. Mungu Ibariki East Africa.
Saumu Maqbul ndugu zangu waisilamu.
 
peleka upumbavu wako kwenu hamna cha maana chochote mlichofaidika zaidi ya siasa za Ukabila na kuendelea kumwezesha Mkikuyu kuendelea kuwatawala! Siasa za Tanzania haziwahusu
 
peleka upumbavu wako kwenu hamna cha maana chochote mlichofaidika zaidi ya siasa za Ukabila na kuendelea kumwezesha Mkikuyu kuendelea kuwatawala! Siasa za Tanzania haziwahusu

hahaha boss, unajua vizuri mimi huwa sikujibu eh? katafute watoto wenzako mbadilishane matusi, hapo mimi sipo. IGNORED
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…