Mara nyingi tunajiona tuko salama, tunafikiri mabadiliko, kanuni, sheria za kigandamizi zinazofanywa na watawala hazituhusu sisi hasa hawa watumishi wa uma; watu wa magereza, wanajeshi, maaskari police, watumishi wa almashauri, walimu, mahakimu n.k.
Hutashangaa kusikia kada hizi zikikemea wanaopinga kikokotoo kipya, hutashangaa kusikia wakiwapinga na kuwabeza wanaotaka katiba mpya, hutashangaa wakiwabeza wanaowauliza watawala dhalimu maswali magumu na ya msingi kuhusu kubinafsishwa kwa bandari zetu zote na baadhi ya misitu na hifadhi za wanyama. Kinyume utawasikia wakisema hao wana wivu, hawa ni wapinga serikali, hawa hawana akili, wametumwa na mabeberu, hakika watatuhalibia amani na upendo wa nchi yetu
Sasa leo yamemkuta aliyekuwa mtumishi wa Magereza ndugu Shamte (56) staff Surgent alipojikuta akiambulia kiinua mgongo (malipo ya pension ya kustaafu) cha shilingi 21 millioni badala ya shilingi 55 millioni aliyotarajia baada ya kuitumikia serikali kwa miaka zaidi ya 33.Mstaafu huyo aliyasema hayo baada ya kutembelea ofisi za Magazeti ya mwananchi juzi.
"Najiona mfungwa mtarajiwa baada ya kubakia na shillingi 10 millioni kwani shillingi 10 millioni nyingine zimekatwa baada ya kuwa nilikopa chama cha ushirika wa Akiba na Mikopo cha watumishi wa Jeshi la Magereza" alitoa masikitiko yake bwana Shamte akitumia mfano wa mateso ya watu aliokuwa akiwachunga kila siku wakati akifanya kazi gerezani, kwani anajua machungu ya kuwa mfungwa. "Nilitegemea nikanunue shamba la kulima mazao niweze kujisitili baada ya kustaafu sasa haiwezekani, sioni mbele maisha yatakuwaje" bwana Shamte akitoa sentensi kuashiria kukata tamaa ya maisha
"Wewe ndugu, utaratibu wa malipo ya pensheni halipi CGP, waziri husika au katibu mkuu, utalipwa kulingana na michango yako" hayo ndiyo majibu ya kifupi na kukatisha tamaa aliyopewa mtumishi mstaafu ndugu Shamte kutoka kwa wakuu wake baada ya kupata ujumbe wa kiasi atakacholipwa.
Swali la kujiuliza ni, je ? tuko akina Shamte wangapi? akina shamte ambao tunakubali kila kitu watawala wanachopitisha kwa manufaa yao, akina shamte tunaokuwa wa kwanza kuwanyooshea vidole wale wachache wenye akili timamu na uthubutu wa kuhoji haya mabadiliko dhalimu kwa niaba na manufaa yetu, utasikia hawana akili hao, utasikia wamechanganyikiwa hao, nakwambia utasikia wametumwa na wazungu , mabeberu. Wengi wetu tunafikili madhara ya sheria dhalimu , mabadiliko kandamizi haya hayatuhusu sisi, yanawahusu wale tu wanaolalamika.
Hakika bwana shamte amekumbuka shuka wakati kunakucha , amekumbuka jinsi alivyokuwa akiwadharau waliokuwa wakipinga kikokotoo kipya na pengine alishiriki kuwahadhibu walipopelekwa gerezani alikokuwa akifanya kazi, hakika alimalizia kwa kutubu na kusema "Wakati watu wanalia kuhusu kikokotoo nilikuwa naona kawaida,sasa nimeona ukali wake.
Swali la msingi ni, Je...? wewe na mimi tumejifunza nini katika kisa mkasa hiki cha mstaafu Shamte?