Rubawa
JF-Expert Member
- Dec 25, 2015
- 2,055
- 3,254
NA MOHAMMED ABDULRAHMAN
Kiswahili ni lugha inayozungumzwa katika kanda ya Afrika Mashariki kuanzia Somalia hadi Msumbiji na ni lugha ya mawasiliano kwa sehemu kubwa ya kanda hiyo. Tanzania ndiyo iliokuwa msitari wa mbele katika kuitumia lugha kama lugha ya taifa na ilioweza kuwachanganya watu wa makabila mbali mbali na kujihisi ni wamoja. Katika miaka ya hivi karibuni Kiswahili kimeanza pia kupewa kipa umbele kwa kasi kubwa katika nchi jirani, zikiwemo Kenya ambako pamoja na kuwa lugha inayotumika na kuenziwa eneo la pwani nchini humo lakini ilikuwa haikupewa uzito sehemu ya bara. Kwengineko ni Uganda, Rwanda,´Burundi na kwa kiwango fulani hata Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Kiswahili kinazungumzwa pia , sehemu za Malawi, Msumbiji, Somalia na miongoni mwa washwahili walioko maeneo ya bara Arabu hasa Oman na Umoja wa Falme za Kiarabu ambako idadi yao si ndogo. Lakini kwa bahati mbaya nchini Tanzania , nchi ambayo imekuwa ikiangaliwa kama kioo panapohusika na hifadhi ya Kiswahili na maendeleo yake, Kiswahili kimeanza kutumiwa vibaya na si jambo la kuficha kuwa kinaporomoka. Matumizi mabaya yanaathiri Kiswahili sanifu. Kwa mtazamo wangu kuna sababu nyingi za Kiswahili kuanza kuporomoka na katika hili, wanasiasa , vyombo vya habari na taasisi zinazosimamia lugha hii wanachangia huu ninaouita mimi mchafukoge. Huko kwenye mitandao ya kijamii nako ndiyo hakusemeki.
Nianze na wanasiasa:
Mara nyingi nimekuwa nikifuatilia hotuba , mahojiano mijadala bungeni na pia hutuba za wanasiasa wengi bila ya kujali vyama vyao na wataalamu wa sekta mbali mbali . Kwanza kumeibuka mtindo ambao mimi nauita “kasumba,” wa kuchanganya Kiswahili na Kiingereza , wakati lugha ya taifa ni Kiswahili na wengi walioko maeneo ya vijijini Kiingereza hakieleweki vizuri. Lakini kama hayo hayatoshi, baadhi ya wakati utagundua mzungumzaji anavuruga lugaha zote mbili. Lazima niungame kunatokea wakati ambapo katika kuzungumzia hoja au mada fulani, linahitajika neno la kitaalamu ambalo halipo katika Kiswahili au maelezo yake yataeleweka vizuri zaidi kwa kutumia Kiingereza.
Lakini swali hasa ni, kwanini patumiwe lugha ya kigeni pasina sababu ? Huenda ni kwasababu ya kile nilichokiita kuwa kasumba-udhaifu wa kujiona labda bila ya kuzungumza kimombo utakuwa huna hadhi na kusahau kwamba hadhi na heshima yako mbele ya yule anayekusikiliza ni ufasaha wa kujieleza na kutetea hoja zako . Pia kuna mtindo mpya ya kutumiwa lugha za kikabila kwenye kadamnasi ya mchanganyiko wa watu, mfano mikutano ya hadhara . Hili pia linaonekana kwa wanasiasa. Hatari yake inajenga tabia ya kuanza kujinasabisha na ukabila badala ya utaifa. Ikiwa kuanzia Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere hadi mawaziri wake na wanasiasa miaka yopte wakizungumza Kiswahili fasaha na kuchangia kuimarisha mshikamano, iweje sasa iwe vyenginevyo ?
Vyombo vya habari:
Vyombo vya habari navyo vimeingia katika mkumbo wa kukikoroga Kiswahili na hali ni ya kusikitisha . Wapo wanaohoji kuwa utitiri wa redio na magazeti bila ya mpangilio ni sababu moja wapo. Mimi siipi uzito sana hoja hiyo, kwani naamini sababu kubwa ni kuwa tasnia ya habari imevamiwa na na wasio na maarifa ya kutosha kuanzia katika taaluma yenyewe hadi lugha . Kunakosekana mtenganisho wa kuwa mtangazaji na mwandishi habari au yote mawili. Mtu yeyote anaweza kujinadi kuwa ni mwandishi habari ili mradi tu amefanikiwa kuingia katika taaluma hiyo.
Kisichoopewa uzito ni umuhimu wa mtu kuwa na uwezo wa kuitumia lugha kwa kuzingatia matamshi safi, sahihi pamoja na mpangilio wake, kwa maneno mengine Kiswahili sanifu. Katika kukivuruga Kiswahili, siku hizi baadhi ya watangazaji na waandishi habari hutumia maneno kama,“Kujiuzuru badala ya kujiuzulu, Amemdhurumu badala ya Kumdhulumu au Taaruma badala ya Taaluma,“ na kwa hakika orodha ni ndefu. Sambamba na dosari hizo kumeibuka matumizi ya maneno kama Kuzungumzaga, kwendaga, kumuoneshaga .
Hizi Ga ,Ga zimeanzanazo kutawala kwa kasi . Katika baadhi ya vyombo vya matangazo kupitia mitandao wa kijamii mbali na dosari hizo kuna tatizo pia la kuchanganywa Kiswahili na Kiingereza na kwa kweli bila ya kutafuna maneno wakati mwengine lugha zote mbili hutumiwa viba , kama si katika mpangilio wa matumizi yake basi matamshi ya maneno . Niliwahi kumsikia mtangazaji mahiri mkongwe Charles Hilary ambaye tulikuwa pamoja Deutsche Welle kabla ya yeye kuhamia BBC akilikemia wimbi hili na kuliita kuwa janga. Jee wahariri wako wapi ? Ninakiri kwamba kuna lugha ya vijana na mitaani na ni kitu cha kawaida kutokeza maneno mapya , lakini kama wasemavyo wahenga ,“kila kitu kina mahala pake.“ Hatari ya matumizi mabaya ya kiswahili na umuhimu wa kukidumisha Kiswahili sanifu imewahi kuzungumzwa na Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete.
Alitoa mfano wa utumiaji wa neno “Dhumuni“ na kuweka wazi kwamba neno sahihi ni “Madhumuni . Neno hilo linatumiwa sana siku hizi sawa na “Dhebu“ badala ya “Madhehebu.“ Pia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa kuhusu maendeleo ya lugha ya Kiswahili mjini Unguja 2018, Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein alielezea kusikitishwa kwake na jinsi maneno yanavyotumiwa mahala sipo na kupotoshwa maana halisi. Akatoa mfano wa neno“Uzalishaji.“ Alisema siku hizi utasikia, "Kiwanda cha kuzalisha viatu," wakati matumizi sahihi ni kiwanda cha“kutengeza“ viatu.
Viko wapi vyombo na taasisi husika:
Swali kubwa ni viko wapi vyombo na wataalamu wanaohusika na maendeleo na hifadhi ya lugha ya Kiswahili, kama Baraza la Kiswahili la Taifa ? Kuwajibika kwa vyombo hivi kunaonekana kuzorota zaidi kinyume na ilivyokuwa miaka ya 1960 hadfi 1990 kuachiwa hali hii iendelee ni ni sawa na kutowaenzi wale waliotoa mchango mkubwa kuanzia waandishi vitabu hadi watunzi wa mashairi, sio tu katika kuiendeleza bali kusaidia kuipa nafasi yake stahiki katika jukwaa la Kimataifa.
Kwa Tanzania nikiwadhukuru wachache ni pamoja na Marehemu Shaaban Robert, Mathias Mnyampala, Abdulbari Diwani , Sheikh Mohamed Ali, mshaii Sadan Abdul Kandoro pamoja na Suleiman Hega kupitia vipindi vyake vya redio. Mbali na waandishi vitabu vya Kiswahili wakiwemo , kutoka Zanzibar marehemu Mohamed Said Abdullah maarufu Bwana Msa, Adam Shafi na Profesa Said Ahmed Khamis . Kenya mwandishi na mshairi Profesa Ahmed Sheikh Nabahany , Abdullatif Abdullah na wengineo.
Fahari ilioje kuona Kiswahili leo ni lugha ya kimataifa , lugha pekee ya kiafrika inayotumiwa katika Umoja wa Afrika na kinasomeshwa karibu katika Vyuo vikuu kote duniani. Wakati umewadia wa kutafakari juu ya hatari inayoikabili lugha hii adhimu. Kusema “ Sisi Kwetu Tunasema Hivi,“ sio sahihi. Kilicho sahihi ni kuzingatia utaratibu na matumizi ya Kiswahili sanifu.
Kuna msemo Kiswahili kina wenyewe, Lakini pia Kiswahili ni cha kila anayekizungumza kwa ufasaha na kuzingatia matumizi sahihi lugha hii na utaratibu wake. Kandoni mwa hayo yote, pana haja kubwa ya kuziba pengo la ukosefu wa waalimu wa kiswahili waliobobea kuanzia shule za msingi hadi sekondari . Lugha ni urithi wa taifa. Hivyo ndivyo nionavyo .
Raia Mwema/Twitter: mamkufunzi, Baruapepe:mamohamed55@hotmail.com
Sent using Jamii Forums mobile app