Wakati Yanga inashinda goli moja dhidi ya Namungo zilipigwa nduru sana

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
FT Simba(mwenyeji) 1 Namungo(Mgeni) 1

Narudia kusema tena na ntazidi kusema Ingekuwa ni Simba timu pendwa ya Baba/TFF wangekutana na ratiba ile ya yanga wangedondosha pointi zote washukuru TFF wanawapendelea waziwazi kwa kuwapa ratiba soft.

Baada ya Yanga kupata Ushindi wa goli moja dhidi ya Namungo wakiwa na kocha Cedric Kaze watu hasa mashabiki wa Simba walipiga nduru sana mtaani kwamba Yanga Mbovu, Yanga imeshuka kiwango maneno chungu mzima wakisahau wao bado hawajakutana nao tukumbuke hapo Yanga ilitoka kugawa vipigo vizito vya tano tano.

Leo waliokuwa wanapiga kelele Yanga imebahatisha ushindi wa goli moja dhidi ya Namungo ndio hao wameishia kugawana pointi pale Uhuru Stadium wajuvi wa mambo walisema usitukane mto kabla ya kuvuka mamba almanusura Viboko watoboe mtumbwi leo.

Kwa ushauri tu Simba wachaneni na Uswahili na Propaganda za Kina Ahmed Ally mpira siku hizi ni Sayansi.

Ikisema Roma imesema.
 
Timu ya Rais wa TFF, Simba ni km CHADOMO, vilalamishi, ila ni kwasababu ya historia ya kuundwa kwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…