GE2025 Wakatoliki Dar Kuombea Watu Waliofariki Kipindi Cha Uchaguzi Mkuu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,933
Taarifa iliyotolewa na Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, imeeleza Askofu Mkuu Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, OFMCap, amewaalika Mapadri, Watawa na Waamini wote kushiriki Misa Maalum ya kuwaombea Wafu itakayoadhimishwa Jumatatu, Novemba 10, 2025.

"Mhashamu sana Jude Thaddaeus Ruwa'ichi OFMCap, anawaalika Mapadri, Watawa na Waamini Walei wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam kuadhimisha Misa ya Wafu kwa nia ya kuwaombea pumziko la milele ndugu zetu Marehemu waliouawa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025; aidha katika Misa hiyo pia iwepo nia ya kuwaombea uponaji wote waliojeruhiwa katika tukio hilo" imeeleza taarifa hiyo

Taarifa hiyo imefafanua zaidi kuwa, Parokia zote na Vituo vyote vya Kanisa ndani ya Dar es Salaam vitaadhimisha misa hiyo kwa nia hiyo maalum

Aidha, Askofu Mkuu Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi ametoa wito kwa waamini wote kuendelea kusali kwa ajili ya haki na amani nchini Tanzania.
​
 
Jambo jema. Majimbo mengine yafanye hivi. Walau itasaidia kupunguza chuki.
 
Piga msitari hapo kwenye “kuendelea kuombea HAKI na AMANI nchini “
 
Kanisa la makafara hili
Unahamasisha watu kuandamana na kuleta vurugu, wanashughulikiwa halafu unakuja kukenua mapengo hapa eti tuwaombee...
Nyokonyokoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…