Wakatoliki Tujifunze: Aina za Kanisa na Rehema "Indulgeo"

Wakatoliki Tujifunze: Aina za Kanisa na Rehema "Indulgeo"

Alfred

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2008
Posts
2,093
Reaction score
2,843
Ndugu Zangu Katika Kristu “Tumsifu Yesu Kristu

Kama Mafundisho ya Kanisa Yasemavyo Kuna aina Tatu za Kanisa
1.Kanisa la Mbinguni
2.Kanisa la Duniani
3.Kanisa la Toharani

Pia kwa Imani yetu wakatoliki tunaamini Mtu akifariki yaani “Marehemu” ana sehemu tatu za kwenda Nazo ni

1.Mbinguni
2.Jehanam
3.Toharani


Wakatoliki tunaamini Marehemu hupitia “Toharani” ili kuondolewa au kusamehewa adhabu ya dhambi zake zilizosamehewa kabla ya kuingia peponi, marehemu akiwa toharani Husafishwa, husafishwa kwa moto ili awe safi kuingia katika ufalme wa Mungu


Leo Nataka Tuzungumzie Rehema (Indulgence), Tafadhali Msichanganye na Huruma (Mercy).


Rehema ni nini?

Rehema au indulgence kwa Kiingerea au Indulgeo kwa Kilatini ni msamaha wa adhabu zinazotokana na dhambi zilizosamehewa

“Temporal Punishments” ni ni matokeo ya dhambi tulizotenda hata baada ya Kusamehewa, unaweza kuipata duniani au toharani

Rehema ni kwa ajili ya mtu au marehemu aliyeko toharani

Ili kupata Rehema Muumini atubu dhambi zake na afanye malipizi


*Rehema inatolewa na Kanisa Kwa Mamlaka ambayo Kanisa imepewa na Mungu

(Mamlaka ya Ufunguo) pia kwa Ushirika wa Kanisa na Watakatifu!

Kuna Aina Mbili za Rehema

1.Rehema Kamili
Ni ondoleo au msamaha wa adhabu zote za dhambi zilizosamehewa.
2.Rehema Pungufu
Ni ondoleo au msamaha wa baadhi ya adhabu za dhambi zilizosamehewa.

Unapataje Rehema?

1.Ungama Kwa Padre
2.Timiza Malipizi
3.Usitende Dhambi

PIA
1.Kufanya Hija
2.Kushiriki Misa na ekaristi takatifu
3.Kusali kwa Nia ya Baba Mtakatifu
4.Kusali Njia ya Msalaba

*Ukitimiza Masharti yote utapata Rehema Kamili

*Ukitimiza Pungufu utapata Rehema Pungufu

NOTE: Siku ya ijumaa au ijumaa kuu unaweza Kupata Rehema Kamili!



360_indulgences_0219.jpg



ALFRED “Devout Catholic”
 
Pamoja sana el padrino..
Proudly Catholic
 
Pia kwa Imani yetu wakatoliki tunaamini Mtu akifariki yaani “Marehemu” ana sehemu tatu za kwenda Nazo ni

1.Mbinguni
2.Jehanam
3.Toharani
 
Back
Top Bottom