Wakazi adai alikuwa anafanya kazi kwa Donald Trump

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Posts
5,107
Reaction score
10,969


Msanii wa muziki wa Hip Hop, Wakazi amedai wakati yuko masomoni nchini Marekani alishawahi kufanya kazi kwenye Hoteli ya mgombea Urais wa sasa wa nchi hiyo kupitia chama cha Republican, Donald Trump.
Rapper huyo amedai kazi ya hoteli ni kazi ambayo ilimpa nafasi ya kukutana na mastaa wengi zaidi wakiwemo Kanye West, Floyd Maywether, Diddy na Wengine Kibao.

“Nilikuwa tu Door man (Mfungua milango) shughuli zangu ni Front Desk, kwa hiyo nikapata kazi Trump Tower ya Donald Trump, yeye mwenyewe aliwahi kuja siku ile tu inafunguliwa ila watoto wake nimeshakutana nao sana” Wakazi alikiambia kipindi cha Campus Vibes cha Times FM.

Wakazi aliendelea kusimulia kuwa tabia kubwa ya Bilionea Trump, ni kusoma Magazeti kila siku alfajiri saa 11 na dakika 45, hivyo alikuwa akitumwa kumpelekea Magazeti Chumbani kwake kila siku asubuhi lakini kwa masharti ya kutokushikana mikono.

“Nilikuwa nampelekea Magazeti kila siku saa 11 ukifika hamuongei wala kushikana mikono, anafungua milango alafu wewe unayaweka chini, ilikuwa ni tabia yake huwa hapendi Kushake ‘hands’.”

Katika hatua nyingine rapa huyo ameongeza, kuna kipindi aliamua kuacha kazi kwa tajiri huyo ili ajihusishe zaidi na muziki huku mcheza kikapu mtanzania Hashim Thabeet akimsaidia baadhi ya mahitaji.
 
leo nimeona picha na mrembo wetu wa tz ameshikwa kiuno na trump
 
Picha ziko wapi sasa...yani uuunge ungeee marekani ukae New York City.....huyu atakua alikua Idaho huko aiseee...desiyn kama kigoma flani hivi....
 
Wivu wako umekufanya uone ni issue... Jamaa kazungumzia tajriba yake, akiwa 'mfungua mlango' wewe unaleta mbofumbofu zenye wivu ndani yake.
kwani akiwa huko kafanya kazi sehemu moja...mbona hizo hajazisema?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…