Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Rapa Wakazi ametoa kauli kali akiwakosoa wasanii kwa kutojitambua na kutojihusisha na masuala muhimu ya kijamii. Katika andiko lake, alisisitiza kuwa wasanii wengi wamepoteza dira yao ya kuwa kioo cha jamii na badala yake wanataka kuwa matajiri wakifuatilia mafanikio ya msanii maarufu Diamond. Wakazi alieleza kuwa wasanii hawapo tayari kushiriki katika mapambano ya kijamii, badala yake wanajipendekeza kwa viongozi ili kupata manufaa binafsi.
Aidha, alieleza kuwa wengi wao hawazingatii hata masuala yanayowahusu moja kwa moja, hawajiungi na vyama vya kulinda maslahi yao, na wana mikataba mibovu inayowakandamiza. Pia, aliwashauri wanaharakati kuunga mkono wasanii wanaopigania haki badala ya kuwasusia wale ambao hawasimami na jamii.
Wakazi alihitimisha kwa kusema kuwa wasanii wana nafasi kubwa katika mapambano ya mabadiliko, lakini itakuwa vigumu kufanikisha hili kama njaa itaendelea kuwa tatizo.
Soma => Nay wa Mitego: Asilimia kubwa ya wasanii ni wa Serikali. Tuache uoga wa kukemea mambo ya kikatili na kutegemea Wasanii kupaza sauti